Na Mahmoud Zubeiry, Johannesburg, Afrika Kusini
IMEWEKWA AGOSTI 10, 2013 SAA 4:40 ASUBUHI
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Kipre Herman Tchetche jana alifuatwa kwa ajili ya mazungumzo na klabu ya Blomofontein Celtic mjini hapa, ambao wameonyesha nia ya dhati zaidi kutaka kumsajili, ingawa na Mamelodi Sundwons nao pia wamezungumza naye.
Nyota huyo wa Ivory Coast jana alitoka katika hoteli ya Rundburg Towers mjini hapa kwenda kukutana na Rais wa Blomofentein, Jimmy Augousti na kocha Muingereza, Stewart Hall alimruhusu kwenda akijua hakuna lolote linaloweza kufikiwa bila kuhusishwa uongozi wa timu na wamiliki.
Kipre hakuwa tayari kuelezea kwa undani juu ya mazungumzo yake na Rais huyo wa klabu hiyo- ingawa habari zinasema Blomofontein sasa watawasiliana na uongozi wa Azam kwa ajili ya mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu.
Mapema Jumatano, baada ya mechi dhidi ya Mamelodi, Kipre alifuatwa na viongozi wa klabu hiyo na kufanya mazungumzo kwa ufupi. Pamoja na Kipre, wachezaji wengine ambao wamezivutia klabu za hapa ni kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’.
Lakini klabu nyingi zimekuwa zinakata tamaa ya kuchukua hatua zaidi- baada ya kuambiwa Azam FC kwa sasa ni moja klabu tajiri sana Afrika na imewekeza, ikiwa na mipango ya kuwekeza zaidi, ili kutawala soka barani siku zijazo.
BIN ZUBEIRY inafahamu- msimamo wa wamiliki wa timu kwa sasa ni kutouza mchezaji wake yeyote mzuri, kwani wanataka kuimarisha timu ifanye vyema kwenye michuano ya Afrika na pia kuchukua ubingwa wa Bara msimu huu, baada ya kuukosakosa mara mbili mfululizo.
Azam imekuwa ya pili katika Ligi Kuu ya Bara kwa misimu miwili mfululizo iliyopita, kwanza nyuma ya Simba SC na baadaye nyuma ya Yanga SC- lakini msimu huu dhamira kuu ni kuwa mbele ya vigogo hao wa soka Tanzania.
Mwaka huu ikicheza kwa mara ya kwanza Kombe la Shirikisho, ilifanikiwa kufika hatua ya 16 Bora na kutolewa na AS FAR Rabat ya Morocco kwa jumla ya mabao 2-1. Azam ingeweza kusonga mbele hadi hatua ya makundi, kama John Bocco ‘Aedebayor’ asingekosa penalti zikiwa zimesalia dakika nane mchezo kumalizika mjini Rabat.
Azam ipo hapa tangu Agosti 3, kwa ajili ya kujiandaa na msimu- ambapo wataanza na mechi ya kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC, Agosti 17, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwaka jana, Azam FC ilifungwa 3-2 na Simba SC katika mechi ya kuwania Ngao, licha ya kuongoza kwa mabao 2-0 hadi mapumziko, lakini kocha Stewert amepania kubeba ‘Ubao’ safari hii.
Tangu iwasili hapa, Azam, ambayo imekuwa ikijifua katika viwanja vizuri vya Chuo Kikuu cha Wits, ikitokea kwenye hoteli ya nyota tano, Rundburg Towers, imekwishacheza mechi tatu na kufungwa mbili, ikishinda moja.
Ilifungwa 3-0 katika mchezo wa kwanza na Kazier Chiefs, ikashinda 1-0 katika mchezo uliofuata na Mamelodi kabla ya jana kufungwa 2-1 na Orlando Pirates, wakati Jumatatu itacheza mechi ya mwisho na Moroka Swallows kabla ya Jumanne kurejea Dar es Salaam.

![]() |
| Anatakiwa; Kipre Herman Tchetche anatakiwa na Blomofontein Celtic ya Afrika Kusini. |
PROGRAMU YA AZAM AFRIKA KUSINI:
AGOSTI 3, 2013:
Kuwasili J’burg kutoka Dar
AGOSTI 4, 2013:
Mazoezi (Chuo Kikuu cha Wits)
AGOSTI 5, 2013:
Azam 0-3 Kaizer Chiefs
AGOSTI 6, 2013: Mazoezi (Chuo Kikuu cha Wits)
AGOSTI 8, 2013:
Mazoezi (Chuo Kikuu cha Wits)
AGOSTI 10, 2013: Mazoezi (Chuo Kikuu cha Wits)
AGOSTI 11, 2013:
Mazoezi (Chuo Kikuu cha Wits)
AGOSTI 12, 2013:
Azam Vs Moroka Swallows
AGOSTI 13, 2013: Kuondoka Johannesburg kurejea Dar es Salaam
Kuwasili J’burg kutoka Dar
AGOSTI 4, 2013:
Mazoezi (Chuo Kikuu cha Wits)
AGOSTI 5, 2013:
Azam 0-3 Kaizer Chiefs
AGOSTI 6, 2013: Mazoezi (Chuo Kikuu cha Wits)
AGOSTI 7, 2013:
Azam 1-0 Mamelodi Sundwons AGOSTI 8, 2013:
Mazoezi (Chuo Kikuu cha Wits)
AGOSTI 9, 2013:
Azam 1-2 Orlando PiratesAGOSTI 10, 2013: Mazoezi (Chuo Kikuu cha Wits)
AGOSTI 11, 2013:
Mazoezi (Chuo Kikuu cha Wits)
AGOSTI 12, 2013:
Azam Vs Moroka Swallows
AGOSTI 13, 2013: Kuondoka Johannesburg kurejea Dar es Salaam
Mapema Jumatano, baada ya mechi dhidi ya Mamelodi, Kipre alifuatwa na viongozi wa klabu hiyo na kufanya mazungumzo kwa ufupi. Pamoja na Kipre, wachezaji wengine ambao wamezivutia klabu za hapa ni kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’.
Lakini klabu nyingi zimekuwa zinakata tamaa ya kuchukua hatua zaidi- baada ya kuambiwa Azam FC kwa sasa ni moja klabu tajiri sana Afrika na imewekeza, ikiwa na mipango ya kuwekeza zaidi, ili kutawala soka barani siku zijazo.
BIN ZUBEIRY inafahamu- msimamo wa wamiliki wa timu kwa sasa ni kutouza mchezaji wake yeyote mzuri, kwani wanataka kuimarisha timu ifanye vyema kwenye michuano ya Afrika na pia kuchukua ubingwa wa Bara msimu huu, baada ya kuukosakosa mara mbili mfululizo.
Azam imekuwa ya pili katika Ligi Kuu ya Bara kwa misimu miwili mfululizo iliyopita, kwanza nyuma ya Simba SC na baadaye nyuma ya Yanga SC- lakini msimu huu dhamira kuu ni kuwa mbele ya vigogo hao wa soka Tanzania.
Mwaka huu ikicheza kwa mara ya kwanza Kombe la Shirikisho, ilifanikiwa kufika hatua ya 16 Bora na kutolewa na AS FAR Rabat ya Morocco kwa jumla ya mabao 2-1. Azam ingeweza kusonga mbele hadi hatua ya makundi, kama John Bocco ‘Aedebayor’ asingekosa penalti zikiwa zimesalia dakika nane mchezo kumalizika mjini Rabat.
Azam ipo hapa tangu Agosti 3, kwa ajili ya kujiandaa na msimu- ambapo wataanza na mechi ya kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC, Agosti 17, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwaka jana, Azam FC ilifungwa 3-2 na Simba SC katika mechi ya kuwania Ngao, licha ya kuongoza kwa mabao 2-0 hadi mapumziko, lakini kocha Stewert amepania kubeba ‘Ubao’ safari hii.
![]() |
| Anazitoa udenda; Salum Abubakar 'Sure Boy' anazitamanisha klabu za hapa |

.png)