IMEWEKWA AGOSTI 10, 2013 SAA 3:50 ASUBUHI
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester City, Mario Balotelli sasa amefungua 'ghala' la kufuga nguruwe na amemtambulisha nguruwe wake mpya mdogo katika famili yake ya wanyama hao haramu kwa Waislamu.
Mchezaji huyo wa AC Milan ameandika kwenye ukurasa wake wa Twetter juu ya nguruwe huyo mpya mdogo wa kike, aliyempa jina Super.
Ameposti picha Twitter, Balotelli akiwaambia wafuasi wake Milioni 1.1: "Hatimaye nguruwe wangu mdogo amewasili! Ana miezi miwili tu (kuzaliwa)! Ni wa kike, lakini nimemuita SUPER!'

Kitu kipya: Mario Balotelli amemtambulisha 'Super' nguruwe mpya katika famili yake ya wanyama hao

Akimpa jina la utani alilopewa akiwa Man City, inasemekana kuna utata kidogo juu ya rafiki yake huyo mpya kama ni wa kike au wa kiume.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ametweet: "Haswa siwezi kuiona jinsia yake, hivyo nafikiri ni mwanamke ahahahaha, lakini labda ni mwanaume! Ahahah'.




.png)