• HABARI MPYA

    Thursday, August 01, 2013

    BAYERN MUNICH YAILAZA SAO PAOLO 2-0 NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA AUDI, SASA KUUMANA NA MAN CITY

    IMEWEKWA AGOSTI 1, 2013 SAA 7: 00 USIKU
    KLABU ya Bayern Munich imeifunga Sao Paulo mabao 2-0 katika michuano yao ya Kombe la Audi Cup na kuungana na Manchester City katika fainali itakayopigwa Uwanja wa Allianz Arena.
    Sasa kocha Pep Guardiola anajiandaa kukabiliana na timu yenye safu kali ya ushambuliaji, City ambayo mapema iliikung'uta AC Milan 5-3 katika mchezo wa kwanza.
    Mabao yote Bayern yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji Mario Mandzukic na kinda Mitchell Weiser ingawa na wageni walipata nafasi ya kufunga baadaye, lakini kipa Rogerio Ceni akakosa penalti. Thiago Alcantara aliachwa nje na kocha Guardiola.
    Goalscorers: Mandzukic (above) and Mitchell Weiser (below) are congratulated after their goals
    Wafungaji wa mabao: Mario Mandzukic (juu) na Mitchell Weiser (chini) wakipongezana
    Goalscorers: Mandzukic (above) and Mitchell Weiser (below) are congratulated after their goals
    Katika mchezo ambao walifungwa mabao 4-2 na Dortmund kuwania Super Cup ya Ujerumani, Thiago, ambaye alikuwa anawaniwa na Manchester United majira haya ya joto, alipigwa kibao na Guardiola.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BAYERN MUNICH YAILAZA SAO PAOLO 2-0 NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA AUDI, SASA KUUMANA NA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top