IMEWEKWA AGOSTI 10, 2013 SAA 3:32 ASUBUHI
KLABU ya Barcelona inataraji David Luiz kuiambia Chelsea Jumatatu kwamba anataka kuondoka kujiunga na mabingwa hao wa Hispania.
Barca ilipeleka ofa ya kwanza kumtaka beki huyo wa kimataifa wa Brazil ambayo ilipigwa chini Jumatano na kocha Jose Mourinho akwaonya wasijisumbue kurejea na ofa nyingine.
Pamoja na hayo, Barcelona inashawishika Mourinho anatafuta njia za kupandisha dau la mchezaji huyo na inatumai Luiz ana nia ya kujiunga nao- hivyo kusaidia majadiliano kuendelea.

Anasubiri mchezo: Barca inataraji Luiz kuwasilisha maombi ya kuondoka siku zijazo kulazimisha kuondoka
Beki wa Liverpool, Daniel Agger anabakia kuwa chaguo lao mbadala, lakini ametangazwa kuwa Nahodha mpya Msaidizi wa Anfield, akichukua nafasi ya Jamie Carragher.
Wiki hii, Mourinho amemuambia kocha wa Barca, Tata Martino kwamba hawawezi kubadili mawazo yao kwa vyovyote na akajaribu bahati yake kwingine.
"Hii ofa? Ni kupoteza muda kwao," alisema Mourinho.
"Ushauri wangu kwao ni kwenda kwa mchezaji wa pili katika orodha yao, kwa sababu wanapoteza muda wao. Hatutaki kupoteza wachezaji wetu wazuri. Hakuna nafasi,".


Tatizo la safu ya ulinzi: Kocha wa Barca, Martino anaweza kumgeukia beki wa Liverpool, Agger iwapo atamkosa Luiz


.png)