IMEWEKWA AGOSTI 10, 2013 SAA 3:20 ASUBUHI
KUNA mvutano uliopo kati Yanga na TFF kuhusu haki ya matangazo ya TV, ambapo TFF wameingia mkataba na Azam TV. Sina sababu ya kurudia yale yote yanayosemwa kwa pande zote tatu, pamoja na taarifa nyingi zilizopo chini ya kapeti ingawa pia sio vizuri kuamini habari za chini ya kapeti, ingawa sio vizuri pia kuamini hizo taarifa za chini chini, ila pia si za kuzibeza.
Yanga wameweka wazi na wanaona haikuwa sawa na TFF walijibu madai ya Yanga, timu nyingine zote zimeridhia kasoro Yanga peke yao wamekataa na wamesema michezo yao isionyeshwe- na TFF bila hiyana wamekubali, lakini michezo ya ugenini si mali yao.
Sina sababu ya makala hii kumtafuta mchawi kuwa mkweli nani au nani yupo sahihi, nawaomba sasa Yanga na TFF wakae chini wamalize huu mgogoro kwa manufaa ya mpira wa miguu na Maendeleo yake kwa Taifa kwa ujumla.
Wakutane, wazungumuze na wote wawe na nia ya dhati kabisa ya kuumaliza mgogoro. Kwa kweli kwa mgogoro huu uliopo sasa, pande zote tatu zitaathirika kwa namna moja au nyingine.
Kama kweli Yanga watakuwa hawana haki ya kuzuia mechi zao za ugenini zisionyeshwa, watakuwa na hasara kubwa sana, kwani ngumu kwa mtazamo wangu kupata udhamini wa michezo ya nyumbani tu ambayo itakuwa michezo saba kwa na upewe fedha, zaidi ya Azam TV sio rahisi na kama hutapata mdhamini na michezo yako ya ugenini ikaonyeshwa, hiyo ni hasara zaidi.
Pia kwa upande wa TFF, wana wajibu wa kumlinda mdhamini wa haki za matangazo, kwani Yanga ina mashabiki wengi kuliko, timu nyingine zote Tanzania kwa takwimu zinazotokana na mapato ya mlangoni na michezo mingi ya Yanga ya nyumbani itachezwa Uwanja wa Taifa kama hakutakuwa na mabadiko.
Ni Uwanja mzuri, hata mabango yataonekana kwa uwazi zaidi, hivyo hiyo ni fursa kwa Azam TV iliyowekeza mabilioni ya fedha katika mradi huo- na tofauti na hivyo, nao wataathirika kwa namna moja au nyingine.
Kwa uhakika, huu mgogoro hauna masilahi kwa maendeleo ya mpira wa miguu kwa ujmla, nawaombeni sana tena sana Yanga, Azam TV na TFF kaeni chini mtatue mgogoro huu.
Kila upande uondoe dhana ninayoiona ya kuungwa mkono, kwa TFF wanaona wanaungwa mkono na timu 13 zinazishiriki Ligi Kuu na kwa upande wa Yanga wanaona wanaungwa mkono na wanachama wao- na hii ni hatari pia kwa usalama wa watu wengine wanaotofautiana na uongozi kwa swala hili.
Nasema ni hatari kwa sababu akiwa ni mwanachama mwenzako kuna uwezekano wa kufanyiwa fujo na kama siyo mwanachama mwenzako, ataonekana ni adui wa maendeleo ya Yanga.
Naye uwezekano wa kufanyiwa fujo ni mkubwa sana.
Kwa taswira iliopo ya mkutano wa 18/08/2013 ni kuwashitaki watu wote waliotofautina na Yanga kuhusiana na haki ya matangazo ya TV kwa wanachama wake, kwa wachache wao wenye jazba ni ngumu wakati mwingine wadhibiti au kudhibiti hasira zao na ninashauri Yanga na TFF waache kutunishiana misuli, badala yake busara zaidi ipewe nafasi.
Kwangu mimi naona ufumbuzi wa mgogoro huu utapatikana kama pande zote tatu, yaani Yanga, TFF na Azam Tv watakuwa na nia ya dhati.
Ni Muhimu sana kukubali pande zote tatu kuingia kwenye mazungumzo, kuwe na msimamizi au mwongoza mazungumzo au usuluhishi, amabaye hatakuwa na masilahi na mgogoro huu kwa namna moja au nyingine, kwani wao wanaonekana kutokuaminiana kila mtu anamwambia mwenziwe ana ajenda ya siri asiyotaka kuiweka wazi- hivyo ni vizuri kuwepo na msuluhishi asiyeegemea upande wowote.
Pande zote tatu tuangalie masilahi ya taifa zaidi kuliko masilahi ya mtu mmoja mmoja au kikundi cha mtu fulani. Kuacha huu mgogoro ukaendelea ni kama kutunza bomu kwenye kibuyo kisubili kulipuliwa.
Hakuna sababu ya kuiambia Yanga iamue inavyoona inafaa, sioni kama ni sahahi na hii inaonekana kuna udhaifu pia wa kanuni za TFF.
Si suala la Yanga kuonyeshwa michezo yao au kutoonyeshwa- suala ni kanuni zinasemaje, kama hazipo zitengenezwe na sio zitengenezwe kwa malengo ya Yanga tu, iwe ni fundisho kwa siku za mbeleni.

.png)