• HABARI MPYA

    Saturday, August 10, 2013

    ARSENAL YAIKUNG'UTA MAN CITY 3-1 LEO

    IMEWEKWA AGOSTI 10, 2013 SAA 3:01 USIKU
    USHINDI wa mabao 3-1 ambao Arsenal imeupata leo kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Helsinki dhidi ya Manchester City katika mchezo wa kirafiki unamaanisha The Gunners wanaweza kuendelea na maisha  bila Luis Suarez.
    Arsene Wenger anahaha kusaka saini ya mshambuliaji huyo asiyefurahia maisha Liverpool akiwa ana matumaini makubwa ya kumpata Suarez, licha ya ofa yake ya Pauni Milioni 40 kupigwa chini.
    Katika mchezo wa leo, mabao ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott dakika ya tisa, Aaron Ramsey dakika ya 59 na Olivier Giroud dakika ya 62, wakati bao la City limefungwa na Negredo dakika ya 80.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny/Fabianski dk46, Sagna/Jenkinson dk73, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta/Perez dk68, Ramsey/Hayden dk88, Wilshere/Cazorla dk46, Podolski/Giroud dk46, Oxlade-Chamberlain/Zelalem dk74 na Walcott 
    Manchester City: Hart, Zabaleta (Richards 46), Kompany, Lescott/Boyata dk86, Clichy, Milner/Navas dk46, Fernandinho/Rodwell dk80, Toure/Garcia dk68, Silva, Negredo/Jovetic dk68 na Dzeko/Nasri dk46.
    Top Gunners: Theo Walcott and Aaron Ramsey were two of Arsenal's scorers in their friendly win
    Wakali wa Gunners: Theo Walcott na Aaron Ramsey waliifungia Arsenal leo
    Top Gunners: Theo Walcott and Aaron Ramsey were two of Arsenal's scorers in their friendly win
    Mashabiki wa Arsenal
    Rampaging: Yaya Toure tries to get away from Aaron Ramsey
    Yaya Toure akipambana na Aaron Ramsey
    Spanish connection: David Silva (right) and Mikel Arteta jump for the ball during the second half
    David Silva (kulia) na Mikel Arteta wakigombea mpira
    Neat: Theo Walcott kept his cool to lift the ball over Joe Hart for Arsenal's opener
    Theo Walcott akimtungua Joe Hart kuifungia Arsenal bao la kwanza
    Tussle: Pablo Zabaleta and Alex Oxlade-Chamberlain (right) battle for possession
    Pablo Zabaleta na Alex Oxlade-Chamberlain (kulia) wakipambana
    Footballing centre half: Vincent Kompany tries to launch an attack from the back for City
    Vincent Kompany akijiandaa kuanzisha mashambulizi
    Ready? Arsenal fans parade a Finland flag through Helsinki ahead of the kick-off
    Tayari? Mashabiki wa Arsenal wakitamba na bendera ya Finland mjini Helsinki kabla ya mechi
    Hands on: Carl Jenkinson accidentally catches Samir Nasri in the face with an arm
    Carl Jenkinson akipambana na Samir Nasri 
    Easy as that: Aaron Ramsey capped a fine display by rounding Joe Hart to score Arsenal's second
    Kilaini namna hiyo: Aaron Ramsey akimtungua kipa Joe Hart
    Frustrations: City playmaker David Silva remonstrates with the referee after a decision in the first half
    Amepagawa: Kiungo wa City, David Silva aliudhiwa na uamuzi wa refa kipindi cha kwanza
    Looking sharp: Walcott was involved in two of Arsenal's three goals
    Walcott ameifungia Arsenal leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENAL YAIKUNG'UTA MAN CITY 3-1 LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top