• HABARI MPYA

    Sunday, June 24, 2012

    NAFTALI, BANKA, THOM MAURICE WAIBEBA BANDARI MOMBASA


    Dadid Naftali

    Na Prince Akbar
    TIMU ya soka ya Bandari ya Mombasa, Kenya imemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Daraja la Kwanza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu inayoongoza ligi hiyo Kariobang Sharks jana.
    Beki wa zamani wa Simba, David Naftali ameiambia BIN ZUBEIRY kutoka Kenya jana kwamba mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Bandari, Mbalak Sport.
    “Kwa sasa timu yetu ipo vizuri baada ya kusajiliwa Mohamed Banka, Meshak Abel na Thomas Maurice, japo anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja,”alisema Naftali na kuongeza; “Kaka siyo siri combination ya midfield mimi na Banka ni hatari, imekuwa gumzo kuanzia Nairobi mpaka Mombasa, Sasa tunashika nafasi ya pili kwa pointi 38, tunazidiwa pointi mbili tu na anayeongoza ligi, Sharks,”alisema.
    Kwa sasa ligi hiyo inaenda mapumziko na wachezaji wote w2qa timu hiyo wa Kitanzania waterejea nyumbani kwa mapumziko mafupi.
    Banda ilishuka daraja msimu uliopikta na inapigana ili msimu ujao irejee Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAFTALI, BANKA, THOM MAURICE WAIBEBA BANDARI MOMBASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top