• HABARI MPYA

    Friday, May 04, 2012

    SIMBA WATWAA UBINGWA NJE YA UWANJA, AZAM FC WAONYESHWA HAWAJUI


    Kikosi cha Simba kilichotwaa ubingwa leo kikiwa kambini Zanzibar, baada ya Mtibwa Sugar kuituliza Azam kwa kichapo cha mabao 2-1.

    SIMBA leo wanaanza kushangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya Azam FC kufungwa mabao 2-1 na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Simba ina pointi 59, ambazo sasa haziwezi kufikiwa na timu yoyote msimu huu na imebakiza mechi moja dhidi ya watani wa jadi, Yanga Jumapili ambayo kwao itakuwa ya kulinda heshima tu.
    Lakini Azam tayari imejihakikishia nafasi ya pili kwenye ligi hiyo na hivyo kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani.
    Waliokuwa mabingwa watetezi Yanga, hawana tena chao- kwani hata wakiifunga Simba keshokutwa watabaki nafasi ya tatu tu, hivyo mwakani hawavuki mipaka ya nchi.
    Tumaini pekee la Yanga kucheza michuano ya Afrika mwakani ni iwapo Simba SC itaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu- ikiwa imebakiza mitihani miwili kufikia mafanikio hayo.
    Inatakiwa kuitoa Al Ahly Shandy ya Sudan- na baadaye iitoe timu itakayokutana nayo kwenye mchujo wa kuwania kucheza hatua hiuyo, ambayo itakuwa imetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa.
    Hapo, Tanzania itakuwa na nafasi mbili kwenye Kombe la Shirikisho mwakani, kwa mujibu wa kanuni mpya za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
    Tayari Simba imeifunga Shandy mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza na inahitaji sare katika mchezo wa marudiano wiki ijayo ili kusonga mbele.
    Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Mtibwa walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Awadh Issa dakika ya 25, wakati kipindi cha pili, Wakata Miwa hao wa Manungu waliokuwa wanashangiliwa kwa nguvu na mashabiki wa Simba, walipata bao la pili dakika ya 59, mfungaji akiwa ni Juma Abdul.
    Awadh alifunga bao lake akiunganisha kona iliyochongwa na nyota wa mchezo wa leo, Juma Abdul ambaye naye alifunga bao la pili kwa mpira wa adhabu, baada ya Luckson Kakolaki kumchezea rafu Vencent Barnabas Saramba. John Raphael Bocco 'Adenauor' aliifungia Azam bao la kufutia machozi.

    MABINGWA WA JUMLA LIGI KUU:
    1965 : Sunderland (Dar es Salaam)
    1966 : Sunderland (Dar es Salaam)
    1967 : Cosmopolitans (Dar es Salaam)
    1968 : Yanga
    1969 : Yanga
    1970 : Yanga
    1971 :  Yanga
    1972 : Yanga
    1973 : Simba
    1974 : Yanga
    1975 : Mseto SC (Morogoro)
    1976 : Simba
    1977 : Simba
    1978 : Simba
    1979 : Simba
    1980 : Simba
    1981 : Yanga
    1982 : Pan African
    1983 : Yanga
    1984 : Simba
    1985 : Yanga
    1986 : Tukuyu Stars (Mbeya)
    1987 : Yanga
    1988 : Coastal Union (Dar es Salaam)
    1989 : Yanga
    1990 : Simba 
    1991 : Yanga
    1992 : Yanga
    1993 : Yanga
    1994 : Simba
    1995 : Simba
    1996 : Yanga
    1997 : Yanga
    1998 : Yanga
    1999 : Mtibwa Sugar (Morogoro)
    2000 : Mtibwa Sugar (Morogoro) 
    2001 : Simba
    2002 : Yanga
    2003 : Simba
    2004 : Simba
    2005 : Yanga
    2006 : Yanga
    2007 : Simba (Ligi Ndogo)
    2008 : Yanga
    2009:  Yanga
    2010: Simba SC
    2011: Yanga SC
    2012: Simba SC


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    3 comments:

    Anonymous said... May 4, 2012 at 9:06 PM

    Hiyo ndo simba bwana!!!!! utaipenda tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    Anonymous said... May 4, 2012 at 9:50 PM

    simba!!!!!!!!!!!!!!!!! utaipenda tu

    mohamed hassan said... May 4, 2012 at 11:19 PM

    ONGERA SIMBA SC. KUWA BINGWA 2012 WAKATI MMEBAKIZA MCHEZO MMOJA MKONONI.
    MECHI ILIYOBAKI NI KAMA MAZOEZI YA KUJIANDAA KUCHEZA NA WA-SUDANI.

    Item Reviewed: SIMBA WATWAA UBINGWA NJE YA UWANJA, AZAM FC WAONYESHWA HAWAJUI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top