• HABARI MPYA

  Monday, January 02, 2017

  SENEGAL YACHUKUA WAKONGWE MBENGUE NA SOW AFCON 2017

  TIMU ya taifa ya Senegal imewaorodhesha wazoefu beki Cheikh Mbengue na mshambuliaji Moussa Sow katika kikosi cha wachezaji 23 wa mwisho watakaokwenda Gabon kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
  Wawili hao walikosa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwezi Novemba nchini Afrika Kusini, lakini wote wamerudi kucheza fainali zao za tatu za AFCON.
  Henri Saviet wa St Etienne pia amerejeshwa na kocha Aliou Cisse kwa ajili ya michuano hiyo ya wiki tatu, ambako Senegal imepangwa Kundi B dhidi ya Algeria, Tunisia na Zimbabwe.
  Moussa Sow ameingia kwenye kikosi cha mwisho cha Senegal kitakachokwenda Gabon kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika

  Kikosi hicho kinahusisha wachezaji 12 waliocheza fainali zilizopita za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea, ambako Senegal ilishindwa kuvuka raundi ya kwanza licha ya kutaabiriwa kufika mbali awali.
  Senegal itaanza kampeni zake kwa kumenyana na Tunjisia Januari 15 mjini Franceville.
  Kikosi kamili cha Senegal kinaundwa na makipa: Abdoulaye Diallo, Khadim Ndiaye na Pape Seydou Ndiaye.
  Mabeki: Saliou Ciss, Lamine Gassama, Kalidou Koulibaly, Cheikh Mbengue, Kara Mbodj na Zargo Toure.
  Viungo: Mohamed Diame, Pape Kouly Diop, Idrissa Gana Gueye, Cheikhou Kouyate, Pape Alioune Ndiaye, Cheikh Ndoye na Ismaila Sarr.
  Washambuliaji: Famara Diedhou, Mame Biram Diouf, Diao Balde Keita, Moussa Konate, Sadio Mane, Henri Saivet na Moussa Sow.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SENEGAL YACHUKUA WAKONGWE MBENGUE NA SOW AFCON 2017 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top