• HABARI MPYA

  Monday, January 02, 2017

  AZAM NA YANGA WAANZA KUKINUKISHA MAPINDUZI LEO

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi 2017 inaendelea leo kwa mechi mbili za Kundi B kupigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mabingwa wa zamani wa michuano hiyo, Azam FC watacheza na Zimamoto kuanzia Saa 10:00 jioni, kabla ya mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga kumenyana na Jamhuri ya Pemba kuanzia Saa 2:30 usiku. 
  Mechi hizo zinafuatia mechi za ufunguzi za Kundi A zilizoanza Ijumaa Taifa Jang’ombe ikiilaza 1-0 Jang’ombe Boys.
  Yanga kumenyana na Jamhuri ya Pemba kuanzia Saa 2:30 usiku

  Na jana wenyeji KVZ walianza vibaya baada ya kufungwa 2-0 na mabingwa watetezi, URA wakati vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba waliichapa 2-1 Taifa Jang'ombe.
  Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu Mzambia, George Lwandamina imepania kufanya vizuri kwenye michuano ya mwaka huu baada ya kutokuwa na matokeo mazuri kwa miaka minne iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM NA YANGA WAANZA KUKINUKISHA MAPINDUZI LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top