• HABARI MPYA

    Thursday, July 09, 2015

    TIMU YA AKINA BIN KLEB, BIG BON YATWAA KOMBE LA MWEZI MTUKUFU DIAMOND

    Na Princess Asiaa, DAR ES SALAAAM
    TIMU ya Chole United imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya kuifunga mabao 2-1 Saggar katika fainali usiku wa kuamia jana Uwanja wa shule ya Diamond, Upanga, Dar es Salaam.
    Katika mchezo huo ambao mgeni rasmi alikuwa Diwani wa Upanga Mashariki (CCM), Sultan Ahmed Salim, shujaa wa mechi alikuwa ni Abaly mfungaji wa mabao yote ya Chole moja kila kipindi.
    Nahodha wa Chole United, Moudy Mass akiinua Kombe la ubingwa wa mashindano ya mwezi mtukufu usiku wa kuamkia jana Uwanja wa shule ya Diamond, Upanga, Dar es Salaam, baada ya kuifunga Saggar 2-1
    Washindi wakiwa na Kombe na Medali zao baada ya mechi 

    Chole United ambayo iliingia baada ya kuwafunga ndugu zao Chole Rangers kwa bahati, baada sare hadi kwenye penalti, kufuatia sare ya 2-2 Jumatatu, pia imetoa mfungaji bora wa mashindano, Lutfy Bin Kleb aliyefunga mabao manne sawa na Mohammed Sadat.
    Saggar iliyoitoa DFC United kwa bao 1-0 katika Nusu Fainali, ilishindwa kufurukuta mbele ya Chole United iliyoongozwa na Nahodha Moudy Mass.
    Wafadhili wa Chole, Abdallah Bin Kleb na Big Bon wamempongeza Lutfy kwa kuwa alicheza mechi zote kama beki wa kushoto, lakini bado akaweza kuwa mfungaji bora.
    Mabingwa; Kikosi cha Chole United kilichotwaa Kombe la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
    Lutfy (kushoto) akipongezwa na kaka yake, Abdallah Bin Kleb ambaye pia ni mmoja wa wafadhili wa Chole pamoja na Big Bon
    Wachezaji wa Chole wakishereheea na mashabiki wao baada ya ubingwa
    Mgeni rasmi akikabidhi Medali kwa washindi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU YA AKINA BIN KLEB, BIG BON YATWAA KOMBE LA MWEZI MTUKUFU DIAMOND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top