• HABARI MPYA

    Wednesday, July 08, 2015

    NGOMA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YANGA SC, APIGA BAO PEKEE, KMKM YALALA 1-0 TAIFA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Mzimbabwe, Donald Ngoma (pichani juu) amefunga bao pekee akiichezea Yanga SC kwa mara ya kwanza ikishinda 1-0 dhidi ya KMKM ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ngoma alifunga bao hilo dakika ya 50 kwa kichwa akimalizia kona maridadi ya kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho.
    Pamoja na kufunga bao hilo, Ngoma alipoteza nafasi zisizopungua tatu za kufunga, wakati Mliberia Kpah Sherman naye pia alipoteza nafasi mbili na Simon Msuva moja.
    Timu zote zilishambuliana kwa zamu vipindi vyote viwili na kivutio zaidi alikuwa ni beki wa kushoto wa Yanga SC, Mwinyi Hajji Mngwali ambaye alionyesha uwezo mkubwa wa kulinda na kusaidia mashambulizi. 
    Mshambuliaji wa Yanga SC, Donald Ngoma akimtoka beki wa KMKM, Mussa Said kulia
    Winga wa Yanga SC, Godfrey Mwashiuya akimtoka beki wa KMKM, Kassim Abdulkadir
    Winga wa Yanga SC, Deus Kaseke akimtoka beki wa KMKM, Sadi Idrissa

    KMKM, mabingwa wa Zanzibar na Yanga SC mabingwa wa Tanzania Bara, wote wanajiandaa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza wiki ijayo Dar es Salaam. 
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Joseph Zuttah, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Mbuyu Twite, Deus Kaseke, Salum Telela/Simon Msuva dk66, Kpah Sherman/Amissi Tambwe dk46, Donald Ngoma/Malimi Busungu dk81 na Godfrey Mwashiuya/Andrey Coutinho dk46.
    KMKM; Nassor Abdullah, Kassim Abdulkadir, Said Idrissa, Khamis Ali, Mussa Said, Ibrahim Khamis, Nassor Ali/Hajji Simba dk54, Tizzo Charles, Juma Mbwana, Fakhi Mwalimu/Maulid Ibrahim dk63 na Matheo Anthony.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGOMA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YANGA SC, APIGA BAO PEKEE, KMKM YALALA 1-0 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top