• HABARI MPYA

    Wednesday, July 22, 2015

    MEMPHIS DEPAY AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO MAN UNITED IKISHINDA 3-1 MAREKANI

    Memphis Depay akimchambua kipa wa San Jose, David Bingham kuifungia Man United bao la pili katika ushindi wa 3-1 asubuhi ya leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    ZIARA YA MAN UNITED MAREKANI 2015 

    Julai 18 Vs Club America (Seattle) ilishinda 1-0
    Julai 22 Vs San Jose Earthquakes (San Jose) 
    Julai 25 Vs Barcelona (Santa Clara) 
    Julai 30 Vs Paris Saint-Germain (Chicago)
    TIMU ya Manchester United imeshinda mechi ya pili asubuhi hii katika ziara yake ya kujiandaa na msimu nchini Marekani baada ya kuichapa mabao 3-1 San Jose Uwanja wa Avaya mjini San Jose.
    Juan Mata alianza kuifungia United dakika ya 32, kabla ya Memphis Depay kufungua akaunti yake ya mabao katika klabu yake mpya kwa bao zuri la pili dakika ya 37.
    San Jose wakafanikiwa kupata bao moja dakika ya 42 kupitia kwa Fatai, lakini nyota anayechipukia vizuri Andreas Pereira akafunga bao zuri la kichwa kuihakikishia ushindi timu ya Louis van Gaal.
    Kikosi cha Louis van Gaal sasa kitamenyana na mabingwa wa Ulaya, Barcelona katika mchezo ujao wa michuano ya Kombe la Mabingwa wa Kimataifa Jumamosi nchini humo. 
    Kikosi cha Manchester United kilikuwa; kipindi cha kwanza; Johnstone, Darmian, Jones, Blind, Shaw, Carrick, Schneiderlin, Young, Mata, Memphis na Rooney.
    Kipindi cha pili: Johnstone, McNair, Smalling, Evans, Blackett, Lingard, Schweinsteiger, Herrera, Pereira, Januzaj na Wilson.
    San Jose Earthquakes: Bingham, Wynne/Koval dk46, Bernardez/Silva dk62, Goodson/Renato dk46, Stewart/Francis dk46, Alashe, Pierazzi/Pelosi dk46, Garcia/Coutadeur dk46, Cato/Thompson dk46, Salinas/Barrera dk46 na Amarikwa/Sherrod dk46, Jahn dk71.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MEMPHIS DEPAY AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO MAN UNITED IKISHINDA 3-1 MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top