• HABARI MPYA

    Tuesday, July 07, 2015

    MEMPHIS DEPAY MPYA WA KWANZA KUANZA MAZOEZI MAN UNITED

    MSHAMBULIAJI Memphis Depay amejiunga na wachezaji wenzake wa Manchester United kwa mara yaa kwanza tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 25 kutoka PSV.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa sura mpya pekee viwanja vya Carrington jana wakati kikosi cha Louis van Gaal kiliporejea mazoezini kabla ya ziara ya Amerika kujiandaa na msimu mpya.
    Depay alipigwa picha akiwa amevalia jezi namba 26 ambayo atakuwa anitumia United na inatarajiwa mashabiki hawatajali hilo zaidi ya kile atakachokifanya uwanjani.
    Memphis Depay (wa pili kulia), akiwa mazoezini na wachezaji wenzake Man United, Wayne Rooney (kushoto), Phil Jones (kulia) na Michael Carrick PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MEMPHIS DEPAY MPYA WA KWANZA KUANZA MAZOEZI MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top