• HABARI MPYA

    Tuesday, July 07, 2015

    MAYWEATHER APOKONYWA MKANDA ALIOSHINDA DHIDI YA PACQUIAO

    BONDIA Floyd Mayweather amepokonywa mkanda wa WBO uzito wa Welter alioshinda dhidi ya Manny Pacquiao- na Anthony Mundine ameomba kuzichapa naye Septemba.
    Mayweather alishindwa kulipa wakati Ijumaa dola za KImarekani 200,000 ambayo ni ada ya mkanda kwa WBO na Kamati imeamua kumvua taji hilo mbabe huyo mwenye umri wa miaka 38. Inamaanisha Timothy Bradley JR anatarajiwa kuvikwa mkanda huo baada ya kumshinda kwa utata Jessie Vargas mwezi uliopita.
    Mayweather bado ana siku 14 za kukata rufaa, ingawa uamuzi hautarajiwi kubadilishwa.

    Floyd Mayweather (kushoto) amevuliwa mkanda wa WBO alioupata kwa kumshinda Manny Pacquiao

    "Kamati ya ubingwa wa dunia ya WBO imeona hakuna namna nyingine zaidi ya kuendelea kumtambua Floyd Mayweather Jr. kama bingwa wa WBO uzito wa Welter duniani na kumvua mkanda kwa kushindwa kutimiza raratibu za mapambano ya ubingwa wa dunia wa WBO," imesema WBO Jumatatu.
    Mayweather bado ni bingwa wa uzito wa Welter ma Super Welter wa WBC na WBA, ingawa mabondia hawaruhusiwi kushikilia mataji ya uzito tofauti.
    Mayweather anatarajiwa kurejea ulingoni kwa mara ya 49 ambalo linaweza kuwa pambano lake la mwisho Septemba na Mundine – mshindani mkuu wa WBC katika uzito wa Super-Welter amemuandikia barua ya wazi bondia huyo kuomba awe mpinzani wake afuataye. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAYWEATHER APOKONYWA MKANDA ALIOSHINDA DHIDI YA PACQUIAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top