• HABARI MPYA

    Wednesday, July 16, 2014

    MALINZI AWAVAMIA GHAFLA DOMAYO NA KIMWAGA CHAMAZI, AWAMWAGIA ZAWADI NA FARAJA TELE

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi leo amewatembelea wachezaji wawili wa Azam FC ambao ni majeruhi, viungo Frank Domayo na Joseph Kimwaga.
    Wawili hao wapo chumba namba 19 katika hosteli za klabu yao, zilizopo Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam baada ya kurejea kutoka kufanyiwa operesheni nchini Afrika Kusini wiki tatu zilizopita.
    Na Malinzi alifika ghafla leo mchana Azam Complex kuwajulia hali nyota hao walio katika wakati mgumu hivi sasa na kuwapa vijizawadi kuwafariji.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi kulia leo amewatembelea wachezaji majeruhi wa Azam, Frank Domayo na Joseph Kimwaga

    Malinzi akawaahidi TFF itaendelea kuwa bega kwa bega na wao kuhakikisha wanapona na kurudi tena uwanjani. Aidha, Malinzi ameipongeza Azam FC kwa kuwa klabu mfano wa kuigwa kwa kuwajali wachezaji wanapokuwa wazima na majeruhi.
    “Nichukue fursa hii pia kuwapongeza wakurugenzi, wamiliki na viongozi wa Azam FC kwa kuonyesha kuwajali wachezaji kwa hali zote, naomba huu uwe mfano wa kuigwa na klabu nyingine zote nchini,”.
    “Siyo mchezaji anakuwa mzuri anapokuwa mzima tu, akiwa majeruhi anatelekezwa, hivyo siyo sawa, huo si utu na si uungwana,”amesema.
    Malinzi amewatembelea wachezaji hao siku nne kabla ya timu ya taifa, Taifa Stars haijacheza na Msumbiji katika mchezo wa kwanza hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Faibali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani.
    Kimwaga aliyeibukia akademi ya klabu hiyo na Domayo aliyesajiliwa msimu huu kutoka Yanga SC, wote walikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kabla ya kuumia. 
    Na wachezaji hao wamemshukuru Malinzi kwa kuwajali na kuitakia kila la heri Stars katika mchezo wa Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AWAVAMIA GHAFLA DOMAYO NA KIMWAGA CHAMAZI, AWAMWAGIA ZAWADI NA FARAJA TELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top