• HABARI MPYA

    Saturday, February 15, 2014

    KIPRE TCHETHE: NIKO FITI SANA, WAMAKONDE WATANIJUA KESHO

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam
    MSHAMBULIAJI tegemeo wa Azam FC, Kipre Herman Tchetche amesema kwamba yuko fiti kwa asilimia 100 kuelekea mchezo wa kesho wa marudiano Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Ferrovirio de Beira.
    Kipre Tchetche akimtoka mchezaji wa Ferroviario katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam. Je, kesho atatikiza tena nyavu za Wamakonde hao Beira?

    Mchezaji huyo kutoka Ivory Coast alifunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 wa Azam kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na kuelekea mchezo wa kesho Beira, anawatia homa sana wenyeji.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana kwa simu kutoka Beira, Kipre anayecheza timu moja na pacha wake Kipre Michael Balou, alisema kwamba anamshukuru Mungu yuko fiti kwa asilimia 100.
    Alipoulizwa kama anaweza kurudia kuwafunga Wamakonde hao na nyumbani kwao pia, mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, alisema inawezekana.
    “Kama Mungu akipenda nitawafunga tena, nachoweza kusema tu namshukuru Mungu nipo fiti kwa asilimia 100 kuelekea mchezo huo,”alisema.
    Baada ya ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita, Azam FC sasa inahitaji sare yoyote kusonga mbele.
    Hata ikifungwa 2-1, 3-2 au kwa tofauti yoyote ya bao moja  na yenyewe ikifunga, Azam pia itasonga mbele kwa faida ya bao la ugenini. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPRE TCHETHE: NIKO FITI SANA, WAMAKONDE WATANIJUA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top