Kikosi chs Yanga SC ambacho kiliifunga Komorozine 7-0 katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam
MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC jioni ya leo wanacheza mechi ya mwisho ya Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Komorozine mjini Moroni.
Yanga SC walishinda mabao 7-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Wacomoro Dar es Salaam Jumapili na leo wanatakiwa kumalizia vyema kazi yao dhidi ya timu hiyo dhaifu.
Iwapo Yanga SC itafanikiwa kukamilisha vyema matokeo ya Randi ya Awali, basi itakutana na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misiri katika Raundi ya Kwanza.
Yanga SC ipo Moroni tangu Alhamisi asubuhi na imekuwa ikijifua vikali kuelekea mchezo wa marudiano.
| | |
|
|
|
0 comments:
Post a Comment