IMEWEKWA AGOSTI 11, 2013 SAA 12:07 JIONI
MABAO mawili ya Mdachi, Robin Van Persie yameiwezesha Manchester United kuilaza 2-0 Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii.
Ushindi huo ni faraja na mwanzo mzuri kwa kocha mpya wa United, David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu mwishoni mwa msimu uliopita.



Ushindi huo ni faraja na mwanzo mzuri kwa kocha mpya wa United, David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu mwishoni mwa msimu uliopita.

La kwanza kati ya mengi? David Moyes akiwa ameshika Ngao ya Jamii, taji lake la kwanza Manchester United

Washindi: Nahodha wa Manchester United, Nemanja Vidic akiinua Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa 2-0

Pulizia hapa: Wachezaji wa Manchester United wakisherehekea ushindi wao leo
Van Persie alifunga bao la kwanza dakika ya saba kwa kichwa cha nguvu, akiunganisha krosi ya Patrice Evra kutoka wingi ya kushoto na akafunga la pili dakika ya 59 baada ya kufumua shuiti lililombabatiza beki wa Wigan, James Perch.
Kikosi cha Man Utd kilikuwa: De Gea, Rafael/Smalling dk16, Jones, Vidic, Evra, Zaha/Valencia dk61, Carrick, Cleverley, Giggs/Anderson dk67, Welbeck/Kagawa dk83 na Van Persie/Januzaj dk84.
Wigan: Carson, Boyce, Perch, Barnett, Crainey, McCarthy/Dicko dk86, Watson/Espinoza dk71, McArthur/McCann dk61, Maloney/Gomez dk71, Holt/Fortune dk61 na McClean/McManaman dk62.

Yuko sawa: Van Persie amefunga mabao mawili leo Manchester United ikiifunga Wigan 2-0 Wembley

La kwanza: Robin van Persie akipiga kichwa kuifungia Manchester United bao la kwanza

Mbele ya mtu: Mholanzi akiunganisha krosi ya Patrice Evra

Furaha: Wachezaji wa United wakimpongeza Van Persie baada ya kufunga bao la kwanza Wembley

Winga mpya wa United, Wilfried Zaha akimtoka Ben Watson

Yowe: David Moyes na Owen Coyle wakiwapigia kelele wachezaji wao kuwapa maelekezo

Van Persie akiifungia Manchester United bao la pili

Beki wa Manchester United, Nemanja Vidic akipambana na Shaun Maloney


.png)