IMEWEKWA AGOSTI 10, 2013 SAA 11:10 JIONI
KOCHA David Moyes sasa amehamishia mawindo yake kwa Luka Modric baada ya kukwama kumsajili kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas.
Kocha huyo wa Manchester United amemuorodhesha kiungo huyo wa Real Madrid katika orodha ya wachezaji wa kusajili.
Modric, mwenye umri wa miaka 27, amekuwa akitakiwa na United tangu enzi za Sir Alex Ferguson ambaye alizidiwa kete na Real Madrid mwaka uliopita.

Luka anayetakiwa United: Modric sasa anatakiwa na kocha wa United, Moyes baada ya kushindwa kumpata Fabregas
Alijiunga na Madrid kutoka Tottenham kwa dau la Pauni Milioni 33 ingawa ameshindwa kung'ara La Liga na mashabiki wa timu hiyo wamempigia kura katika wachezaji wa ovyo waliosajiliwa msimu uliopita.
Pamoja na hayo, kocha Jose Mourinho alimtetea wakati wa maandalizi ya msimu kabla ya Modric kuisaidia Madrid katika Ligi ya Mabingwa wakiifunga United Uwanja wa Old Trafford.
Moyes pia anawataka wachezaji wa Everton, Marouane Fellaini na Leighton Baines, lakini inafahamika hayatakuwa majina makubwa yatakayofurahisha mashabiki wa United.


Anatakiwa: Kocha mpya wa United amepambana sana kuwania saini ya Fabregas, lakini nyota huyo Barca ameamua kubaki Hispania


.png)