• HABARI MPYA

    Monday, August 19, 2013

    BARCA YAUA 7-0, REAL YAPATA USHINDI MWEMBAMBA KWA BETIS...MESSI ATIKISA NYAVU, RONALDO ZAMGOMEA

    IMEWEKWA AGOSTI 19, 2013 SAA 4:50 ASUBUHI
    MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi jana alifunga mabao mawili na kutengeneza lingine kuwasaidia Neymar na kocha wa Barcelona, Gerardo Martino kuanza kazi vizuri kwa ushindi wa 7-0 dhidi ya Levante kwenye Ligi Kuu ya Hispania. 
    Katika mchezo huo ambao Neymar alianzia benchi, mabao ya Barca yalifungwa na Sanchez dakika ya tatu, Messi dakika ya 12 na 42 kwa penalti, Alves dakika ya 23, Pedro dakika ya 26 na 73 na Xavi dakika ya 45.
    Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Valdés, Alves, Piqué, Mascherano, Adriano, Fàbregas, Busquests, Xavi, Pedro/Tello, Alexis/Neymar, Messi/Iniesta.
    Levante: Navas, Navarro, Rodas, Barral, El Zhar, Rubén, Juanfran, Xumetra, Sergio, Pedro López na Simao.
    Running riot: Lionel Messi and Co were lethal in the first match of the La Liga season, scoring six first half goals
    Running riot: Lionel Messi and Co were lethal in the first match of the La Liga season, scoring six first half goals
    Watching on: £50m wonderkid Neymar started the match from the bench
    Watching on: £50m wonderkid Neymar started the match from the bench
    Big entrance: Neymar was a second half substitute but Barca had already taken their foot well off the gas by then
    Big entrance: Neymar was a second half substitute but Barca had already taken their foot well off the gas by then
    In action: Neymar wasn't able to get on the score sheet
    In action: Neymar wasn't able to get on the score sheet

    Nayo Real Madrid imeanza vyema mbio zake za La Liga kwa ushindi mwembamba wa 2-1 dhidi ya Real Betis.
    Jorge Molina aliwatuliza mashabiki Uwanja wa Bernabeu kwa bao la dakika ya 15, kabla ya Karim Benzema kusawazisha dakika 10 baadaye na mchezaji mpya, Isco akafunga la ushindi dakika ya 86.
    Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Lopez, Pepe, Ramos, Khedira/Casemiro, Ronaldo, Benzema/Morata, Özil/Di Maria, Marcelo, Carvajal, Modric na Isco.
    Real Betis: Andersen, Chica, Perquis, Paulao, Nacho, Matilla, Nosa, Verdú, Juanfran, Cedrick na Molina.
    Finally: Isco's late goal gave Real Madrid all three points after a frustrating home performance
    Shujaa: Isco ameifungia bao la ushindi dakika za lala salama Real Madrid 
    Frustrated: Cristiano Ronaldo went close several times but cut a frustrated figure during the match
    Ametoka kapa: Cristiano Ronaldo alipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini akapoteza
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BARCA YAUA 7-0, REAL YAPATA USHINDI MWEMBAMBA KWA BETIS...MESSI ATIKISA NYAVU, RONALDO ZAMGOMEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top