IMEWEKWA JULAI 22, 2013 SAA 8:07 USIKU
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo ameendeleza furaha, baada ya kufunga mabao mawili wakati Real Madrid ikiifumua mabao 6-0 Bournemouth na kumfanya kocha
Carlo Ancelotti awe na mwanzo mzuri kazini katika klabu hiyo ya matajiri.
Ronaldo alifunga dakika ya 22 na 40, wakati mabao mengine ya Real katika mchezo huo wa kujiandaa na msimu yalifungwa na Khedira dakika ya 43, Higuain dakika ya 46, Di Maria dakika ya 69 na Casemiro 82.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Lopez/Fernandez dk45, Carvajal/Casado dk68, Nacho/Quini dk68, Pepe/Mateos dk45, Coentrao/Cheryshev dk45, Modric/Casemiro dk45, Khedira/Illarramendi dk45, Ronaldo/Di Maria dk45, Isco/Kaka dk45, Ozil/Morata dk45 na Benzema/Higuain.
Bournemouth: Flahavan/Jalal dk84, Francis/Purches dk84, Cook/Hughes dk61, Elphick/Addison dk73, Daniels/Stockley dk84, Coulibaly/Harte dk66, Arter/Thomas dk84, MacDonald/Wakefield dk84, Fraser/Matthews dk73, Pitman/Ward dk27 na Grabban/Chiedozie dk66.

Mtu wa mbele: Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real dhidi ya Bournemouth

Ronaldo akimtungua kipa wa Bournemouth, Darryl Flahavan

Real wakishangilia ushindi wao

Amerejea England: Carlo Ancelotti akifurahia mchezo

Zizou: Kocha Msaidizi wa Real, Zinedine Zidane

Gonzalo Higuain akifunga

Isco akiambaa na mpira dhidi ya Shaun MacDonald

Kiungo wa zamani wa Spurs, Luka Modric aling'ara

Tommy Elphick akijaribu kumdhibiti Ronaldo


.png)