IMEWEKWA JULAI 29, 2013 SAA 1:39 USIKU
MANCHESTER United imeibuka na ushindi wa mabao 5-2 leo kwenye Uwanja wa Hong Kong dhidi ya Kitchee na kumpa faraja kocha mpya David Moyes.
Mabao ya United leo yamefungwa na Danny Welbeck dakika ya 16, Smalling dakika ya 22, Fabio dakika ya 26, Januzaj dakika ya 50 na Lingard dakika ya 80, wakati ya wenyeji yamefungwa na Lam dakika ya 53 na Alkande dakika ya 69.
Kikosi cha Man United leo kilikuwa: Amos; Fabio/Rafael dk72, Smalling, Keane, Evra/Buttner dk46, Carrick/Jones dk72, Zaha/Van Persie dk81, Anderson, Cleverley, Young/Lingard dk46 na Welbeck/Januzaj dk46.
Kitchee: Comi, Rodriguez, Rehman, Kei, Alkande, Belencoso, Wai, Annan, Yang na To.

Amefunga: Danny Welbeck ameifungia Manchester United ikiiadhibu Kitchee

Chris Smalling amefunga pia

Robin van Persie aliingia dakika 10 za mwisho

Wilfried Zaha akichezewa rafu na mchezaji wa Kitchee, Daniel Cancela Rodriguez

Adnan Januzaj (katikati) alikuwa kivutio upande wa United kipindi cha pili

Benchi la Ufundi: David Moyes (kulia) akiwa na wasaidizi wake, Ryan Giggs (kushoto) na Phil Neville (wa pili kushoto)

Wachezaji wa Man United wakishangilia

Mikono juu: Mashabiki wa Hong Kong wakiishangilia Manchester United


.png)