IMEWEKWA JULAI 30, 2013 SAA 5:08 USIKU
MCHEZAJI mpya wa Barcelona, Neymar ameanza mazoezi na timu yake hiyo mpya baada ya kukamilisha vipimo vya afya.
Wachezaji wote wa Barcelona waliokuwa kwenye Kombe la Mabara walitipoti jana baada ya mapumziko na Neymar alikuwa miongoni mwao pamoja na Xavi, Andres Iniesta, Cesc Fabregas na Lionel Messi.
Ilikuwa mara ya kwanza kukutana na wachezaji wenzake wapya, baada ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili ghali katika historia ya klabu baada ya Zlatan Ibrahimovic mwaka 2009 kusajiliwa kwa Pauni Milioni 56.
VIDEO Mazoezi ya Barcelona na wachezaji kupimwa afya jana

Si mbaya: Lionel Messi (kushoto) na Neymar (kulia) wakifanya mazoezi pamoja kwa mara ya kwanza

Neymar (kushoto) akiwa na wachezaji wenzake wapya wa Barcelona


Neymar na mchezaji anayetakiwa na Manchester United, Cesc Fabregas (kushoto) wote walikuwa kivutio mazoezini

Nyumbani: Neymar na mchezaji mwenzake wa Brazil, Daniel Alves katika mazoezi ya Barcelona

Karibu: Kipa Victor Valdes akisalimiana na kocha mpya, Gerardo Martino


.png)