• HABARI MPYA

    Thursday, March 22, 2012

    TEVEZ AREJEA NA NEEMA MAN CITY

    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina, Carlos Tevez usiku wa kuamkia leo amerejeana bonge la ngekewa kwenye kikosi cha klabu yake, Manchester City na kuanza vema akiiwezesha timu hiyo kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Chelsea.
    Tevez aliyecheza mechi ya kwanza baada ya miezi sita tangu agome kuingia uwanjani dakika za lala salama kwenye ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich, Septemba mwaka jana kabla ya kuomba radhi wiki mbili zilizopita, aliingia uwanjani dakika ya 66,
    City ikiwa nyuma kwa 1-0, lakini mwisho wa mchezo timu hiyo ikashinda 2-1.
    Bao la ushindi alilofunga Mfaransa, Samir Nasri lilitokana na kazi nzuri ya Tevez na sasa City inazidiwa pointi moja tu na vinara wa Ligi Kuu ya England, Manchester United.
    Chelsea walitangulia kupata bao kupitia kwa Gary Cahill mpira uliombabatiza Yaya Toure.
    City ilisawazisha kwa penalti iliyotupiwa nyavuni na Sergio Aguero, baada ya Michael Essien kuunawa mpira kabla ya Tevez aliyetokea benchi kumpasia Nasri pande la bao la ushindi.
    Ushindi huo unawafanya City wadumishe rekodi yao nzuri kwenye Uwanja wa nyumbani, Etihad msimu huu, hii ikiwa ni mechi ya 20 mfululizo wanashinda, hivyo wanaweka rekodi mpya Ligi Kuu England.
    Kwa Chelsea, hiki kinakuwa kipigo cha kwanza chini ya kocha Roberto di Matteo katika mechi tano za kuwa kwake kazini tangu arithi mikoba ya aliyekuwa bosi wake, Andre Villas-Boas.
    Katika mchezo huo, kikosi cha Man City kilikuwa; Hart, Richards, Zabaleta, Clichy, K Toure, Nasri, Silva/Dzeko dk 76, De Jong/Tevez dk 66, Y Toure, Aguero, Balotelli/Barry dk 46.
    Chelsea: Cech, Ivanovic/Bosingwa dk 21, Cole, David Luiz, Cahill, Ramires, Lampard, Mata Booked, Mikel, Meireles/Essien dk 58, Torres/Drogba dk 73.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TEVEZ AREJEA NA NEEMA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top