• HABARI MPYA

    Saturday, March 31, 2012

    WENGER AFUNGIWA, ATOZWA FAINI


    Wenger

    KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Euro 40 000 (dola za KImarekani 53,100) kwa kuwavaa marefa baada ya timu yake kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na AC Milan mwezi huu.
    UEAFA imesema jana kwamba Mfaransa huyo alikuwa na hatia kwa kitendo chake kwenye mechi ya mwisho ya hatua ya 16 bora Ligi ya Mabingwa, Arsenal ikishinda 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-3.
    Wenger, ambaye awali alifungiwa mechi moja baada ya kwa kosa kama hilo baada ya kutolewa na Barcelona katika hatua kama hiyo, kasha akasimamishwa mechi mbili kupuuza adhabu hiyo, amesema atakata rufaa.
    Akizungumza juzi na Waandishi wa Habari kabla ya UEFA kutangaza adhabu hiyo, Wenger alisema: "Kama nitasimamishwa na haitafafanuliwa, nitakata rufaa moja kwa moja. Naamini kwamba wamewatukuza marefa wa mashindano ya UEAFA na kuwa wasiogusika, kiasi kwamba huwezi hata kuwaambia neno. Kitu pekee wanachoelewa baada ya mechi ni taarifa.
    "Naamini kwamba kama una miaka 25 mfululizo Ulaya, unaweza kuendelea kuwauliza marefa kama unaweza kumuuliza kitu. Ni vigumu kuelewa."
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENGER AFUNGIWA, ATOZWA FAINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top