• HABARI MPYA

    Friday, March 30, 2012

    BARCA NA BILBAO KESHO PATAMU


    Dani Alves

    KOCHA wa Barcelona, Pep Guardiola anaweza kuwapumzisha baadhi ya nyota wake kwa ajili ya mechi ya Jumanne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan katika mchezo wa kehso dhidi ya Athletic Bilbao, Camp Nou.
    Adriano bado yupo nje ya kikosi kwa maumivu ya misuli, wakati Mbrazil mwenzake Dani Alves amemaliza adhabu na amerudi kazini.
    Thiago atacheza baada ya Shirikisho la Soka Hispania kuipangua kadi ya pili ya njano ambayo kiungo huyo aliipata katika mechi dhidi ya Mallorca.
    Ibrahim Afellay ambaye amekosekana kwa muda mrefu amerejea mazoezini na anaweza kuanzia benchi.
    Mikel San Jose amerejea kikosini Athletic Bilbao baada ya kumaliza adhabu na sasa timu hiyo inakwenda Camp Noun a kikosi kamili.
    Vikosi;
    BARCELONA: Valdes, Alves, Mascherano, Pique, Puyol, Xavi, Busquets, Iniesta, Fabregas, Messi na Pedro.
    ATHLETIC BILBAO: Iraizoz, Iraola, Martinez, Amorebieta, Aurtenetxe, De Marcos, Iturraspe, Herrera, Susaeta, Llorente na Muniain.

    JE WAJUA?
    Barcelona imeshinda mechi saba mfululizo La Liga, ikiwa funga wapinzani wake mabao 21-6 kwenye mechi zote hizo.
    Barca hawajafungwa katika mechi 32 zilizopita za La Liga nyumbani na mechi 51 kwa ujumla kwenye mashindano yote Uwanja wa Camp Nou.
    Lionel Messi amefunga mabao 18 katika mechi tisa zilizopita alizoichezea Barca.
    Athletic Bilbao imecheza mechi nne bila kushinda katika in La Liga (sare moja imefungwa tatu).
    Los Leones wameshinda mechi mbili tu kati ya 11 za La Liga ugenini.
    Mara ya mwisho Athletic kushinda Camp Nou ilikuwa 2-1 Novemba, mwaka 2001.
      
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCA NA BILBAO KESHO PATAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top