• HABARI MPYA

    Saturday, March 31, 2012

    RASMI NYOSSO, KAGO HAWAENDI ALGERIA

    JUMA Nyosso ametemwa kwenye kikosi cha kinachoondoka Jumatatu Alfajiri kwenda Algeria kikipitia Misri kwa sababu ameumia kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo dhidi ya African Lyon, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Habari kutoka ndani ya kambi ya Simba zimesema kwamba, wachezaji watakaoondoka ni Juma Kaseja, Derick Walullya, Shomary Kapombe, Kelvin Yondan, Jonas Mkude, Salum Machaku, Patrick Mafisango, Patrick Sunzu, Haruna Moshi ‘Boban’, Emanuel Okwi, Victor Costa, Uhuru Suleiman, Ally Mustafa ‘Barthez’, Amir Maftah, Mwinyi Kazimoto, Obadia Mungusa na Ramadhani Singano.
    Mbali na Nyosso, Juma Jabu pia ni mgonjwa sambamba na Gervais Kago.
    Aidha, pamoja na Simba kushinda mabao 2-0, lakini imebaini pengo la kiungo wake wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango iliyemsimamisha jana kwa muda usiojulikana.
    Kuelekea mechi ya marudiano na ES Setif mwishoni mwa wiki ijayo, Simba lazima iwe na kiungo mtukutu kutoka Rwanda, ambaye aliwashinda Azam FC wakamtua Msimbazi bila dai lolote.
    Habari za ndani kutoka Simba ambazo bongostaz imezipata zimesema kwamba, uongozi wa Simba ulilazimika kumuita Mafisango na kumpa onyo kali juu ya tabia zake na kumrejesha kambini Bamba Beach, Kigamboni tayari kwa safari ya Algeria.
    “Mafisango amerejeshwa na anaondoka na timu kwenda Algeria usiku huu,”kilisema chanzo hicho kutoka Simba.
    Bahati nzuri ni kwamba Mafisango alisimamishwa wakati tayari amekwishakabidhi pasipoti yake kwa uongozi kwa ajili ya kushughulikiwa viza ya safari ya kwenda Algeria.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RASMI NYOSSO, KAGO HAWAENDI ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top