• HABARI MPYA

    Thursday, March 22, 2012

    LIVERPOOL YAPIGWA, ARSENAL YANG'ARA, SPURS SARE


    BAO la Jamie Mackie liliipa ushindi QPR ikitokea nyuma zikiwa zimebaki dakika 13 na kuifunga Liverpool hivyo kufanikiwa kujiondoa kwenye eneo la hatari ya kushuka daraja.

    Sebastian Coates alianza na kufunga na Dirk Kuyt akawafungia Wekundu wa Anfield na kuwaweka mbele kwenye mchezo huo.

    Shaun Derry alirejesha matumaini QPR hkwa bao la kichwa kabla ya mchezaji wa zamani wa Wekundu hao, Djibril Cisse kuwarudi kwa kuwafunga na kufanya 2-2.

    Kosa la Jose Enrique lilimpa nafasi Mackie kufunga bao la ushindi dakika za majeruhi akimtungua kipa Pepe Reina kuipatia bao la ushindi QPR.

    Kipigo hicho kinaiacha Liverpool iwe na matumaini finyu ya kumaliza ndani ya timu za nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, huku Wekundu hao wakiwa wanazidiwa pointi 12 na Tottenham wanaoshika nafasi ya nne, baada ya kipigo hicho cha nne kwenye mechi tano za ligi.

    Katika mchezo mwingine, Arsenal ilishinda 1-0 ugenini dhidi ya Everton na Tottenham Hotspur ililazimishwa sare ya 1-1 na Stoke City.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YAPIGWA, ARSENAL YANG'ARA, SPURS SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top