• HABARI MPYA

    Monday, March 26, 2012

    SASA CHECHE ZOTE LIGI KUU, ASEMA KABURU

    Kaburu kushoto, akiwa na Joseph Kusaga
    MAKAMU Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange, amesema mara baada ya ushindi wa jana dhidi ya ES Setif kwenye Kombe la CAF jijini Dar es Salaam, timu yake sasa inaelekeza nguvu zake kwenye Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
    Akizungumza na wachezaji wa Simba mara baada ya pambano la jana, Kaburu alisema mechi dhidi ya Setif imepita na ni lazima kila mchezaji na kiongozi aelekeze nguvu na akili yake katika pambano la Machi 31 dhidi ya African Lyon ya Dar es Salaam.
    "Wataalamu wanasema mpira ni dakika 90. Zikimalizika hizo maana yake unaangalia nini kilicho mbele yako. Tunashukuru kwamba wachezaji leo mmelinda heshima ya Simba na Tanzania na tunawapongeza sana kwa hilo. Lakini ni lazima tujue bado tuna majukumu mengine," alisema.
    Kaburu alisema ni muhimu kwa Simba kushinda katika mchezo huo kwa vile sasa inashiriki Kombe la CAF baada ya kushika mojawapo ya nafasi za juu katika VPL msimu uliopita.
    "Tukivurunda kwenye ligi maana yake mwakani hatutaweza kushiriki michuano ya kimataifa jambo ambalo halikubaliki ndani ya Simba. Ndiyo maana nasema ni lazima tuelekeze nguvu zetu huko," alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SASA CHECHE ZOTE LIGI KUU, ASEMA KABURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top