• HABARI MPYA

    Wednesday, March 28, 2012

    KIMENUKA SIMBA, WACHEZAJI WADAIWA KUGOMA

    WACHEZAJI wa klabu ya soka ya Simba wamegoma kuingia kambini wakishinikiza kulipwa sehemu ya posho zao baada ya mechi ya kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Es Setif ya Algeria jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
    Kwa mujibu wa mamapipiro.blogspot.com, jana kikosi cha Simba kilitakiwa kuingia kambini Bamba Beach kwa ajilio ya kujiandaa na mechi yake ya ligi kuu bara dhidi ya African Lyon mwishoni mwa wiki lakini baadhi ya wachezaji waligoma kwenda kambini wakishinikizwa walipwe kwanza posho zao.
    Habari zilizopatikana toka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kwamba awali uongozi uliahidi kuwapa shilingi mil.30 lakini walishangazwa na kupatiwa shilingi mil.15 tena ambazo zilitolewa na mmoja ya wadau wa klabu hiyo Azim Dewji kama zawadi ya timu hiyo kuwafunga Es Setif mabao 2-0.
    Fuatilia mamapipiro.blogspot.com kwa taarifa zaidi kuhusu sakata hilo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIMENUKA SIMBA, WACHEZAJI WADAIWA KUGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top