• HABARI MPYA

    Tuesday, March 27, 2012

    SIMBA, YANGA ZAHAMISHIA UPINZANI KOMBE LA FA

    Simba na Yanga uwanjani. Sasa timu hizo zinatarajiwa kuhamishia upinzani wao Kombe la FA
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema michuano ya Kombe la FA itarejea kuanzia msimu ujao na bingwa wake atacheza Kombe la Shirikisho.
    Michuano hiyo ambayo kwa mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2000 na Simba ikawa bingwa, inafanya sasa ushindani uongezeke katika Ligi Kuu.
    Hiyo inatokana na kwamba, bingwa pekee ndiye atacheza michuano ya Afrika, Ligi ya Mabingwa tofauti na ilivyo sasa mshindi wa pili anacheza Kombe la Shirikisho.
    Inawezekana kurejeshwa kwa michuano hiyo kunatokana na ujio wa kampuni ya Ligi Kuu, ambayo inaundwa na klabu za Ligi na ndiyo itakuwa ikiendesha Ligi Kuu, hivyo sasa TFF imeamua kufufua kitegauchumi chake hicho ili angalau ipate chambichambi.
    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limerejesha tena mashindano ya Kombe la FA (TFF) kuanzia msimu ujao 2012/2013 ambapo bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
    Timu zinazotakiwa kushiriki michuano hiyo itakayochezwa kwa mtindo wa mtoano ni zilizosajiliwa ambapo katika maombi yao ni lazima ziambatanishe nakala ya hati ya usajili wa klabu ambayo itatakiwa kuidhinishwa na chama cha mpira wa miguu cha wilaya.
    Ada ya fomu ya maombi ya kushiriki ni sh. 20,000 wakati ada ya mashindano ni sh. 200,000. Usajili wa wachezaji katika Kombe la FA ni ule ule mmoja wa kalenda ya usajili ya TFF ambapo unaanza Juni Mosi na kumalizika Septemba 10.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA, YANGA ZAHAMISHIA UPINZANI KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top