• HABARI MPYA

    Saturday, March 31, 2012

    AZAM KUMKATIA RUFAA CANNAVARO


    Cannavaro akimlinda kipa

    KLABU ya Azam FC inataka kumkatia rufaa beki  Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga kuichezea timu yake katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    Azama wanalalamika kwamba Cannavaro alipewa kadi nyekundu kwenye mechi kati yao na Yanga na alitakiwa kukosa mechi tatu na kwamba adhabu yake haihusiani na wachezaji waliositishiwa adhabu na Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake Alfred Tibaigana.
    Kiongozi mmoja wa Azam, ameiambia bongostaz kwamba hata wakati Tibaigana anatangaza kusitisha adhabu za wachezaji wa Yanga alisema wazi haingilii adhabu zilizotolewa moja kwa moja uwanjani.
    “Mfano sisi, mchezaji wetu Salum Abubakar alipewa kadi nyekundu na akakosa mechi tatu, iweje Yanga wa kwao akose mechi mbili tu?”alilalamika kiongozi huyo.
    Ikumbukwe Azam inawania moja kati ya nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ili iwakilishe nchi katika michuano ya Afrika na ushindi wa jana wa Yanga ni kama unapunguza matumaini yao kupata nafasi hiyo.   
    Simba inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 50, baada ya kucheza mechi 22, wakati Yanga ina pointi 46 baada ya kucheza mechi 21 na Azam imeshuka hadi nafasi ya tatu kwa pointi zake 44

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM KUMKATIA RUFAA CANNAVARO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top