![]() |
| Cristiano Ronaldo aliyefunga bao la kuongoza la Real |
KLABU ya Real Madrid sasa wanaongoza La Liga kwa tofauti ya
pointi sita tu, baada ya usiku wa jana kulazimishwa sare ya 1-1 na Villarreal
na kumaliza mechi ikiwa imepoteza wachezaji wawili wa kadi nyekundu.
Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la 33 msimu huu dakika ya
62, lakini Marcos Senna akasawazisha zikiwa zimebaki dakika nane.
Mambo yaliharibika kwa Real baada ya Sergio Ramos na Mesut
Ozil wote kulimwa kadi nyekundu wakati Jose Mourinho na Msaidizi wake, Rui
Faria walipandishwa jukwaani wote.
Barcelona iliyoifunga Granada 5-3 juzi, imefufua matumaini ya
ubingwa



.png)
0 comments:
Post a Comment