![]() |
| Manchini kulia na Tevez |
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini anatarajia Carlos
Tevez atasaidia sana klabu yake kutimiza ndoto za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu
England baada ya kuanza kazi rasmi jana.
Tevez alikuwa kivutia kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Chelsea akirejea
kwa mara ya kwanza tangu Septemba usiku wa jana Uwanja wa Eastlands, ingawa alianzia
benchi.
Mshambuliaji huyo wa Argentina alimsetia bao la ushindi Samir
Nasri na kuifanya timu yake ipunguze pengo la pointi hadi kubaki moja dhidi ya
vinara wa ligi hiyo, Manchester United.
Sergio Aguero alisawazisha kwa penalti dakika chache tu baada
ya Tevez kuingia hivyo kufanya mchezo uwe 1-1 baada ya Gary Cahill kutangulia
kuifungia Chelsea.
"Nafikiri kwamba ilikuwa muhimu Carlos alitoa pasi nzuri
kwa Samir kufunga na mashabiki wote walifurahia hilo," alisema Mancini.
"Nafikiri Carlos anahitaji muda zaidi, si kazi nyepesi
kwake, lakini ni muhimu kwamba yupo hapa sasa.
"Labda ndani ya siku 10, wiki mbili, atakuwa kwenye
kiwango kizuri. Nafikiri kwamba itakuwa muhimu kwetu.
"Carlos anaweza asiwe katika kiwango chake kwa asilimia 100,
lakini anafahamu soka na alikuwa muhimu kwa sababu alitufanyia jambo kubwa.
"Nimekuwa nikizungumza na Carlos kila siku mwezi huu na
anafahamu alitakiwa kutokea benchi na kucheza dakika 20 katika mchezo huo,
lakini anaweza kucheza zaidi.
"Ni mchezaji muhimu, anahitaji wiki nyingine mbili au
tatu kuwa katika kiwangokizuri, lakini wakati anacheza, anajua wapi pa kupeleka
mpira."



.png)
0 comments:
Post a Comment