• HABARI MPYA

    Thursday, March 22, 2012

    FIFA KUWALIPIA BIMA KASEJA, NSAJIGWA


    Blatter
    JUMA Kaseja na Nsajigwa Shadrack wakiwa wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars watanufaika na ofa ya bima kutoka FIFA.
    Rais wa Shirikisho la Soka la KimataifA (FIFA), Sepp Blatter amesema kwamba bdo hiyo itakuwa ikiwalipia bima wachezajiwa timu za taifa ikiwa ni njia ya kuziridhisha klabu kubwa Ulaya.
    Blatteralisema hayo kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA)- kwamba utaratibu wa bima hiyo utaanza baadaye mwaka huu, , baada ya kuidhinishwa na Wajumbe wa Mkutano wa FIFA mwezi Mei.
    Blatter alisema FIFA itatoa ofa ya bima kwa wachezaji, kwa klabu na vyama vya soka vya nchi kwa mechi zote zilizo chini ya bodi hiyo.
    FIFA inafuata utaratibu wa UEFA, ambayo ilisema Januari italipa bima katika Euro 2012 baada ya ushawishi mkubwa uliofanywa na vyama vya soka Ulaya.
    Wanachama 200 walipiga kampeni nzito ya bima, baada ya Bayern Munich kumpoteza Arjen Robben kwa miezi sita baada ya winga huyo wa Uholanzi kuumia katika Kombe la Dunia mwaka juzi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FIFA KUWALIPIA BIMA KASEJA, NSAJIGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top