Fabrice Muamba ''alifariki'' kwa dakika 78 baada ya kuzirai
uwanjani, amebainisha daktari wa klabu yake ya Bolton Wanderers' Jonathan
Tobin.
Madaktari wanasema kua bado ni mapema kutabiri kama atarejea
uwanjani kucheza soka.
Lakini Dr Tobin amesema ameshangazwa na jinsi mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 23 alivyoweza kuponyoka hadi wakati huu.
Katika mahojiano yenye makiwa, Dr.Tobin amesema hatukua na
hakika, fikra zetu ziliwaza mengine kabisa hatukutazamia kufikia hali hii ya
afuweni kiasi hiki. Ni ajabu.
Muamba alizirai kutokana na kukwama kwa mishipa ya moyo
wakati wa mchuano wa Kombe la FA kwenye uwanja wa White Hart Lane jumamosi
iliyopita.
Dr Tobin ameiambia BBC Michezo kua muuguzi wa klabu ya
Bolton Andy Mitchell alikua wa kwanza kutambua kua mchezaji huyo amezirai.
Nilimsikia akipiga kelele, ''Nendeni uwanjani,nenda
uwanjani'' Hapo ikawa wazi kua kuna hatari pale uwanjani.
Alisema kua Muamba alipewa vifaa viwili vya kumsaidia
kuikunjua mishipa ya moyo mara ya kwanza uwanjani mara ya pili wakati
akipitishwa uwanjani na mara nyingine 13 kwenye gari la wagonjwa kuelekea
hospitali lakini ajabu ni kwamba hakuna hata moja lililofanikiwa.
Moyo wa Muamba ulipoteza mapigo na kwa muda wa dakika 78 hakupumuwa.
Saa mbili baada ya leo kurejesha fahamu, nilimsogelea na
kumuuliza jina lake, akajibu,Fabrice Muamba. Nikasema nasikia wewe ni mchezaji
mzuri wa mpira' akasema'Najitahidi' Nilijihisi chozi likinitoka.''
Mtaalamu ameongezea kusema kua: "singependa kuahidi
muujiza kwa wakati huu lakini kwa hali ilivyo maisha yake hayamo hatarini tena.
Bado ni mapema mno kusema kwa uhakika kama atarudi kucheza
mpira au la.
Dr Sam Mohiddin, mshauri wa masauala ya magonjwa ya Moyo
anayemuangalia Muamba kwa sasa, alisema kua Fabrice amezidi kuonyesha dalili
nzuri za kupona.
Matokeo yake yamekua ya ajabu kutokana na utunzaji usio wa
kawaida. Hali ya afya yake imetushangaza sana.
"Jambo la muhimu ni jinsi alivyotunzwa mara tu
alipoanguka na kuzirai uwanjani, huduma ya haraka na hasa majaribio ya kuamsha
moyo wake uwanjani White Hart Lane na wakati wa kusafirishwa kuelekea
hospitali.
Kwa sasa kurejelea maisha yake ya kawaida ni jambo lenye
uwezekano mkubwa.



.png)
0 comments:
Post a Comment