MWANASOKA wa India, amefariki dunia baada ya kuzimia uwanjani
katika mechi ya ligi ya nyumbani kusini mwa jiji la Bangalore.
D. Venkatesh akiwa na umri wa miaka 27, kiungo wa klabu ya Daraja
la A, Bangalore Mars, aliingia uwanjani akitokea benchi dakika ya 73 na akazimia
mwishoni mwa mchezo, imesema taarifa ya madaktari nchini humo leo.
Vyombo vya habari vya nchini humo vilisema hakukuwa na gari
la wagonjwa na Venkatesh alipelekwa hosptali ya Hosmat Jumatano kwa bajaji.
Taarifa za awali zinasema kwamba uzembe ulichangia kifo chake.
Kifo cha Venkatesh kinakuja siku tatu baada ya kiungo wa
Bolton, Fabrice Muamba kuanguka na kuzimia katika mechi ya Kombe la FA England
akiichezea timu yake dhidi ya Tottenham. Lakini Muamba alinusurika kwa sababu
aliwahi kupelekwa hospitali ya London Chest ambako bado anaendelea na tiba
yakinifu.



.png)
0 comments:
Post a Comment