![]() |
| Dalglish |
WAKATI Liverpool kesho inaingia kwenye mchezo
mwingine wa Ligi Kuu ya England dhidi ya timu iliyo kwenye hatari ya kushuka
daraja, Wigan kwenye Uwanja wa Anfield, mashabiki wa timu hiyo hawajui cha
kufanya kwa kikosi cha kocha, Kenny Dalglish.
Dalglish ameleta Kombe la kwanza tangu mwaka
2006 kwa kuifunga Cardiff kwenye fainali ya Kombe la Ligi na Wekundu hao
watakutana na ama Everton au Sunderland kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA
mwezi ujao.
Lakini mwenendo wa Liverpool katika ligi msimu
wote umekuwa mbovu na kipigo cha mabao 3-2 walichokipata kutoka kwa QPR – wakati
walikuwa wanaongoza 2-0 katikati ya wiki kilikuwa ni cha tisa msimu huu katika
mechi 29.
Wamefungwa mechi nane kati ya 15 za ugenini na
rekodi yao mbele ya mashabiki wao pia inakanganya.
Timu ya Dalglish imefungwa mara moja tu
nyumbani, 2-1 na Arsenal mwanzoni mwa msimu, lakini wamemudu kushinda mechi
tano tu dhidi ya Norwich, Swansea, Blackburn na Stoke ni miongoni mwa timu nane
zilizoondoka na sare Anfield.
Hiyo inawafanya wazidiwe pointi 28 na vinara
wa Ligi Kuu, Manchester United ambao ni wapinzani wao wakubwa na wanaizidi
pointi 19 Bolton inayoshika nafasi ya tatu kutoka mkiani.
Akiwa ametumia kiasi cha pauni Milioni 110 tangu
arejee Anfield Januari, mwaka jana, Dalglish alitarajia mambo makubwa kutokana
na uwekezaji wake.
Baada ya mechi ya QPR, kocha huyo wa Liverpool
alisema; "Tunahitaji kutafuta maswali na kuhakikisha tunakwenda kujifunza
kutokana na hili, tulitawala sehemu kubwa ya mchezo, mipango na uwezo, lakini
(QPR) wameondoka na pointi tatu."alisema.



.png)
0 comments:
Post a Comment