![]() |
| Laurent Koscielny |
WASHIKA Bundi wa London watataka kuonyesha
dhamira yao ya kumaliza ndani ya tatu bora katika msimamo wa Ligi Kuu ya
England kwa kushinda nyumbani dhidi ya Aston Villa kesho.
Ushindi wa nyumbani Jumatano 1-0 dhidi ya
Everton umewafanya vijana wa Arsene Wenger, waliokuwa wanazidiwa pointi 10 wiki
kadhaa zilizopita, kupanda juu ya wapinzani wao katika jiji la London,
Tottenham Hotspur, ambao walilazimishwa sare na toke.
Tottenham watarejea juu iwapo wataifunga
Chelsea kwa mara ya kwanza tangu 1990 kesho, lakini ushindi wa nyumbani Uwanja
wa Emirates, dhidi ya wapinzani walio katika nafasi ya 15, utawarejesha Arsenal
juu tena.
Ushindi dhidi ya Everton ulikuwa wa sita
mfululizo kwa Arsenal katika Ligi Kuu na pia ulikuwa wa kwanza kushinda bila ya
nyavu zao kuguswa kwenye michuano hiyo tangu Februari.
Wenger alianza vibaya msimu huu kutokana na
kuwa na majeruhi wengi, jambo ambalo lilimgharimu kupigwa mabao 8-2 na
Manchester United Agosti.
Baadhi walikwishaanza kumshutumu Mfaransa huyo
kwa kuwa mtu wa kuomba sana msamaha, lakini kurejea kwa mabeki wake tegemeo
kumekuwa chachu ya mafanikio ya siku za karibuni kwa Arsenal.
Thomas Vermaelen, aliyefunga bao pekee la
ushindi dhidi ya Everton, alikosekana muda mrefu na amerejea vema wakati mabeki
wa pembeni Bacary Sagna na Kieran Gibbs nao wameonyesha kurudi vizuri katika Ligi
Kuu wiki za karibuni.
Laurent Koscielny ameonyesha ni kifaa kingine
muhimu kwa safu ya ulinzi ya Arsenal na sasa Mfaransa huyo amewataka wachezaji
wenzake wa Arsenal kudumisha cheche zao.
Per Mertesacker, Jack Wilshere na Emmanuel
Frimpong wataendelea kuwa nje ya Uwanja kwa muda mrefu, lakini Abou Diaby alicheza
kiasi cha saa katika kikosi cha wachezaji wa akiba na Liverpool Jumanne akitoka
kwenye maumivu ya nyama.



.png)
0 comments:
Post a Comment