| Papic akiongoza mazoezi Yanga |
KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam imehamia
kwenye Uwanja wa Tiper, Kigamboni kwa ajili ya mazoezi ya kumalizia msimu huu
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kocha wa Mserbia, Kostadin Bozidar Papic ameiambia
bongostaz asubuhi hii kwamba leo ndio wanaanza rasmi kufanyia mazoezi kwenye
Uwanja huo.
Alipoulizwa sababu za kuhamia huko, kocha huyo
wa zamani wa Orlando Pirates, Kaizer Chiefs na Meritzburg Classic za Afrika Kusini
alisema lengo ni kupata sehemu itakayowafaa bila kuwaathiri wachezaji wao kwa
namna yoyote.
Yanga ipo kwenye vita ya kutetea ubingwa wake
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa
Simba SC inayoongoza na Azam inayoshika nafasi ya pili, wakati mabingwa hao
watetezi wapo nafasi ya pili.


.png)
0 comments:
Post a Comment