![]() |
| Muntari |
KLABU ya Juventus imepigwa faini ya tatu msimu huu kwa vigezo,
baada ya mashabiki wao kufanya hivyo Jumanne katika Nusu Fainali ya Kombe la
Italia dhidi ya AC Milan.
Mamlaka ya soka Italia imepiga faini ya euro 20 000, ambayo
ni mara mbili ya waliyopigwa Juve January baada ya kumfanyia vitendo vya
kibaguzi Mcolombia Pablo Armero wa Udinesena mzaliwai wa visiwa vya Cape Verde,
anayechezea Usiwsi, Gelson Fernandes.
Pia walipigwa faini ya euro 10 000, Oktoba baada ya kufanyiwa
vitendo hivyo dhidi ya Inter Milan.
Kiungo wa Milan, Sulley Muntari wa Ghana na Mholanzi Urby
Emanuelson ndio waliofanyiwa vitendo hivyo vya ubaguzi Jumanne.
Ubaguzi huu unawafanya mashabiki wa Juventus wawe wamekubuhu
kwa tabia hiyo. Walimfayia hivyo mshambuliaji wa Manchester City, Mario
Balotell alipokuwa Inter.
Msimu wa 2008/2009 Juve walilazimika kucheza mechi katika
Uwanja usio na mashabiki baada ya mashabiki wao kumfanyia ubaguzi Balotelli katika
mechi dhidi ya Inter.



.png)
0 comments:
Post a Comment