![]() |
| Aguero |
MSHAMBULIAJI Sergio Aguero amesema Manchester
City hawana mchecheto kuelekea mechi yao na Stoke wakiwania kurejea kileleni
mwa Ligi Kuu.
Kikosi cha Tony Pulis, Stoke kimekuwa nma
matokeo mazuri kwenye Uwanja wake wa Britannia tangu wapande Ligi Kuu mwaka 2008.
City waliambulia pointi mbili tu katika mechi
tatu za Ligi Kuu walizocheza Stoke na pia walitolewa na timu hiyo kwenye Kombe
la FA mwaka 2010.
Kikosi cha Roberto Mancini, pia kilifungwa
kwenye mechi ya mwisho ugenini na Swansea na kupoteza usukani wa Ligi Kuu tangu
Oktoba.
Lakini walipunguza idadi ya pointi
wanazozidiwa na vinara, Manchester United, ambao pia ni mabingwa watetezi na
kubaki moja baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Chelsea katikati ya wiki.



.png)
0 comments:
Post a Comment