| Kikosi cha Simba, Jumapili kitaendeleza ubabe dhidi ya Waarabu? |
JUMAPILI wiki hii, Simba SC ya Dar es Salaam itashuka kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na ESS Setif ya Algeria katika Raundi
ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika, huo ukiwa ni mchezo wa kwanza kabla ya
timu hizo kurudiana wiki mbili baadaye mjini Algiers.
Setif inakuwa timu ya tatu kihistoria kumenyana na Simba SC,
baada ya awali Wekundu hao wa Msimbazi kutolewa na JET katika Klabu Bingwa
Afrika, kabla ba wao kuitoa Al harrach katika Robo Fainali ya Kombe la
Shirikisho Afrika.
Kwa ujumla Simba ni mabalozi wazuri wa Tanzania katika
michuano ya Afrika na wamekuwa wakifanya vema kila wanapomenyana na timu kutoka
Kaskazini mwa Afrika.
Kuelelea mchezo huo, bongostaz inakuletea rekodi ya Simba na
timu za kaskazini mwa Afrika, zikiwemo za kutoka Algeria. Endelea.
LIGI YA MABINGWA
AFRIKA:
MWAKA 1974:
NUSU FAINALI:
Simba Vs Mehallal 1-0:
0-1
(Mehalla ilishinda kwa penalti 3-0, ingawa kuna habari za
kipa wa Simba, Athumani Mambosasa (sasa marehemu) kufanyiwa fujo, wakati wa
upigwaji wa penalti.
MWAKA 1981:
RAUNDI YA PILI:
Simba ilitolewa na JET ya Algeria.
MWAKA 2003:
RAUNDI YA PILI:
Simba (Dsm) Vs Zamalek 1-0
Zamalek (Misri) Vs Simba 1-0
(Simba ilifuzu kwa penaliti 3-2)
MECHI ZA KUNDI A:
Sept. 7/2003:
Simba Vs Ismaili 0-0
Sept. 19/2003:
Ismaili (Msri) Vs Simba 2-1
KOMBE LA WASHINDI
MWAKA 1985
RAUNDI YA PILI
Simba SC Vs Al Ahly (Misri) 2-1 0-2
MWAKA 1996
RAUNDI YA PILI
Simba Vs Al Mokaoulun (Misri) 3-1 0-2 3-3 (Al Mokaoulun
walifuzu kwa faida ya bao la ugenini)
MWAKA 2001
RAUNDI YA PILI
Ismailia (Misri) Vs Simba SC 2-0, 0-1, 2-1
(Mechi ya marudiano ilichezwa mara mbili, baada ya mechi ya
kwanza kuvunjika dakika ya 46, SImba ikiwa inaongoza mabao 2-0, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam(sasa Uhuru). Ismailia walilalamikia hali ya Uwanja kujaa
maji kwamba kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo, hivyo kugoma kucheza
katika mazingira yale na mchezo ukasogezwa mbele kwa siku moja na ndipo wenyeji
waliposhinda 1-0. Hivyo Simba kwa kufungwa 2-0 awali mjini Cairo, walijikuta
wakitolewa kwa matokeo ya jumla ya kufungwa 2-1.
Mchezo wa kwanza ulitawaliwa na vurugu, Polisi walivamia
uwanjani kuwatawanya wachezaji wa Ismailia kwa mabomu ya machozi, waliokuwa
wakimzonga refa kwa madai mashabiki wa Simba walimpiga na chupa mchezaji
mwenzao mmoja, Emad El-Nahhas.
KOMBE LA CAF/SHIRIKISHO:
MWAK 1993
ROBO FAINALI:
Simba Vs USM El Harrach (Algeria) 3-0 0-2 3-2
MWAKA 2010:
RAUNDI YA PILI:
Aprili 25: Simba Vs Haras El Hodoud 2-1
Mei 8: Haras El
Hodood Vs Simba SC 5 - 1


.png)
0 comments:
Post a Comment