• HABARI MPYA

    Tuesday, July 07, 2015

    UGANDA YAFUMULIWA 1-0 NA MALAWI UWANJA WA KAMUZU

    Malawi na Uganda jana Kamuzu
    TIMU ya taifa ya Uganda, The Cranes imechapwa bao 1-0 jana na wenyeji Malawi, The Flames katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Kamuzu Banda mjini Blantyre.
    Kikosi cha Korongo wa Uganda kinachoundwa vijana wa timu ya U-23 kiliwabana Mwale hadi dakika ya 90 wakati mshambuliaji wa wenyeji, Chiukepo Msowoya alipofunga bao hilo pekee na kuinua shangwe za umati uliokuwapo uwanjani.
    Kocha wa Uganda, Mserbia Milutin 'Micho' Sredojevic, aliutumia mchezo huo kama maandalizi ya mechi za kufuzu michuano ya Afrika ya U-23 dhidi ya Misri Julai 18.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA YAFUMULIWA 1-0 NA MALAWI UWANJA WA KAMUZU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top