• HABARI MPYA

    Tuesday, July 07, 2015

    MKWASA AOMBA SIKU 10 MFULULIZO MAANDALIZI DHIDI YA NIGERIA KUFUZU AFCON

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba atahitaji kambi ya siku 10 mfululizo kabla ya kucheza Nigeria Septemba mwaka huu.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Dar es Salaam, Mkwasa amesema wataomba kupata nafasi ya japo siku 10 kufanya mazoezi kwa pamoja kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Nigeria Septemba 5 mwaka huu.
    Mkwasa aliteuliwa kuwa kocha wa Taifa Stars wiki mbili zilizopita baada ya kufukuzwa kwa Mholanzi, Mart Nooij kufuatia matokeo mabaya na katika mchezo wake wa kwanza alitoa sare ya 1-1 na Uganda mjini Kampala.
    Charles Boniface Mkwasa (kushoto) akiwa na Msaidizi wake, Hemed Morocco

    Na leo Nahodha huyo wa zamani wa Taifa Stars amewashukuru Watanzania wote waliowapa sapoti katika mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda uliochezwa mwishoni mwa wiki jijini Kampala.
    Mkwasa amesema kujitolea kwa wachezaji wa Taifa Stars (uzalendo) katika mchezo huo kulipelekea kuwapa wakati mgumu wenyeji, huku watanzania waliojitokeza kuja kushuhudia mchezo huo wakiwashangilia muda wote wa mchezo.
    “Kwa kweli japo timu haikuweza kupata matokezo mazuri sana, lakini tunamshukuru mungu ndani ya wiki moja ya maandalizi, tumeweza kuwapa maelekezo vijana na kuyafanyia kazi, japo wengine walikua wakicheza kwa mara ya kwanza timu ya Taifa walicheza vizuri, kijumla wote kwa pamoja walifanya vizuri sana katika mchezo dhidi ya Uganda” alisema Mkwasa.
    Tanzania imetolewa Raundi ya Kwanza tum bio za CHAN ya mwakani kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya kufungwa 3-0 chini ya Nooij Zanzibar na kutoa sare ya 1-1 Kampala.

    Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine akiwa na Makatibu wa vyama vya soka nchini 

    Wakati huo huo: Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amefungua semina ya makatibu wakuu wa vyama vya soka vya mikoa nchini  (FA's) kuhusu maandalizi ya michuano ya airtel.
    Katika ufunguzi wa semina hiyo, Mwesigwa amewaomba viongozi hao kuzingatia kanuuni na mahitaji katika michuano ya Airtel inayoshirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.
    Mwesigwa amesema viongozi hao wakichagua vijana wenye umri sahihi wa kushiriki kwenye michuano hiyo itatoa fursa kwa makocha kuchagua wachezaji wenye umri halisi kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa nchi yetu.
    Aidha Mwesigwa ameipongeza kampuni ya simu za mkonono ya Airtel kwa kuendesha michuano hiyo kila mwaka, ambapo kwa sasa vijana watatu wapo katika kituo cha mpira miguu kilichopo Dakar - Senegal wanaposoma masomo ya kawaida na kufundishwa mpira wa miguu, huku wakitafutiwa timu za kucheza nje ya Afrika na  kufanya majaribio sehemu mbalimbali Ulaya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWASA AOMBA SIKU 10 MFULULIZO MAANDALIZI DHIDI YA NIGERIA KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top