• HABARI MPYA

    Tuesday, July 07, 2015

    KASEJA AINGIA ‘DARASANI’ KUSOMEA UKOCHA WA MAKIPA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIPA wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Juma Kaseja Juma ni miongoni mwa watakaoshiriki kozi ya makocha wa makipa nchini itakayofanyika Julai 13 hasi 17 mwaka huu mjini Dar es Salaam.
    Kaseja amewika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na klabu zote kubwa nchini Simba na Yanga SC na kwa sasa japo hajatangaza kustaafu soka, lakini ameanza kupata mafunzo ya ukocha.
    Katikati ya msimu uliopita aliomba mwenyewe kujitoa Yanga SC akidai klabu hiyo ilishindwa kutekeleza vipengele vya Mkataba baina yao na tangu hapo amekuwa akifanya mazoezi na timu ya makipa nchini.
    Juma Kaseja (kulia) akiwa na Ally Mustafa 'Barthez' aliyewahi kufanya naye kazi Simba, Yanga na Taifa Stars

    Kozi hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), itashirikisha jumla ya makocha wa makipa 29 wa klabu za Ligi Kuu na timu za taifa na itafanyika katika ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
    Mbani na Kaseja, wengine ni Juma Nassor Pondamali, kocha wa makipa wa klabu bingwa Tanzania Bara, Yanga SC, Rafael Mpangala (Mgambo JKT), Adam Abdallah Moshi (Simba SC ), Khalid Adam Munnisson (Mwadui FC), Choke Abeid (Toto African), Mussa Mbaya (Ndanda FC), Idd Abubakar Mwinchumu (Azam FC), Herry Boimanda Mensady (Tanzania Prisons), Kalama Ben Lwanga (Stand United) na Patrick Mwangata (Mtibwa Sugar).
    Wengine ni Abdi Said Mgude (Coastal Union), Razack Siwwa (African Sports Tanga), Josia Steven Kasasi (Mbeya City), Ramadhani Juma (Kagera Sugar Kagera), Abdallah Said Ngachimwa (JKT Ruvu), John Bosco (Majimaji FC Ruvuma), Fatuma Omary (Twiga Stars), Juma Kaseja Juma (Huru), Athuman Mfaume Samata (Ilala) na Peter Manyika John (Taifa Stars).
    Hussein Tade Katadula (African Lyon), Juma Mohamed Bomba (Kinondoni), Mwameja Mohamed Mwameja (Ilala),  Agustino Malindi Mwanga (Kigoma), Mohamed Abbas Silima (Police SC. Zanzibar), Bakari Ali Kilambo (Kizimbani SC Zanzibar), Hafidh Muhidin Mcha (Zanzibar Heroes), Elyutery Deodatusy Mholery (Kinondoni), Salim Waziri (Tanga)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KASEJA AINGIA ‘DARASANI’ KUSOMEA UKOCHA WA MAKIPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top