• HABARI MPYA

    Thursday, February 13, 2014

    YANGA WAFIKA SALAMA COMORO

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam
    YANGA SC imefika salama mjini Demoni, Comoro tayari kwa mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Komorozine mwishoni mwa wiki.
    Yanga iliyoondoka leo asubuhi, imetua nchini humo ikiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele, baada ya kuichapa Komorozine mabao 7-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam Jumamosi.
    Wachezaji wa Yanga kutoka kulia Mrisho Ngassa, Juma Abdul na Haruna Niyonzima wakiwa Comoro. Chini ni Mrisho Ngassa aliyefunga mabao matatu katika ushindi wa 7-0.

    Iwapo Yanga itahitimisha vyema kampeni yake hiyo, itakutana na mabingwa watetezi, Al Ahly mwezi ujao.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAFIKA SALAMA COMORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top