• HABARI MPYA

    Thursday, February 13, 2014

    KIDUME RAGE AITISHA MKUTANO WA KATIBA SIMBA SC MACHI 16

    Na Asha Muhaji, Dar es Salaam
    MKUTANO Mkuu wa Marekebisho ya Katiba ya klabu ya Simba umepangwa kufanyika Machi 16 mwaka huu badala ya Machi 23 kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
    Uamuzi wa kurudisha nyuma tarehe ya mkutano huo ulifikiwa jana (Jumatano), katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Klabu kilichokutana usiku Makao Makuu ya Klabu, Mtaa wa Msimbazi, jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti, Alhaj Ismail Aden Rage.
    Kidume; Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage ameitisha Mkutano wa marekebisho ya Katiba Machi 16
    Kamati ya Utendaji ya Simba imefikia uamuzi huo kufuatia maelekezo kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyowataka wanachama wake wote mpaka kufikia Machi 20 mwaka huu wawe wameshazifanyia marekebisho katiba zao kwa kuweka kipengele kinachoitambua Kamati za Maadili.
    Simba ilipokea barua hiyo na kwa kuzingatia umuhimu huo Uongozi ukaamua kuifanyia kazi kwa kuitisha Mkutano Mkuu ambapo agenda itakuwa ni moja tu nayo ni marekebisho ya katiba.
    Mbali na kipengele hicho mkutano huo pia utajadili mapendekezo yote ya marekebisho ya katiba yaliyowasilishwa kwa uongozi ili kujadiliwa na kutolewa maamuzi.
    Uongozi wa Simba unawataka wanachama wake kujitokeza kwa wingi siku hiyo kushiriki katika zoezi hilo kwa maslahi ya klabu yao.
    Kwa sasa uongozi unafanya mipango ya kutafuta mahali pazuri utakapofanyika mkutano huo na mara baada ya kupatikana basi uongozi utawatangazia wanachama wake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIDUME RAGE AITISHA MKUTANO WA KATIBA SIMBA SC MACHI 16 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top