KLABU ya Lazio imelazimika kutoa taarifa rasmi na kuchukua hatua za kisheria ili kuthibitisha mchezaji wake wa timu ya vijana ni kinda kweli na hajavuka umri wa miaka 40.
Joseph Marie Minala, anayesema ana umri wa miaka 17, ameibuka na kuposti kwenye mitandao ya kijamii picha zinazomuonyesha akiwa na sura ya kiutu uzima kuliko alivyokuwa mdogo. Nukuu pia zimetokea kwenye vyombo vya habari vya Senegal zikisema kwamba Minala alikuwa ana umri wa miaka 41.
Klabu hiyo ya Italia na wakala wa Minala vimepuuza taarifa kwamba anadanganya, kwa kutoa taarifa kuthibitisha umri wake haliai
Taarifa: Klabu hiyo imetoa taarifa maalum kuhusu umri wa Minala na sasa mchezaji huyo amefuta akaunti zake za Instagram na Facebook
Kazini: Mcameroon huyo alijiunga na Lazio Agosti mwaka jana na amekuwa kivutio katika timu ya vijana ya klabu hiyo
Chumba cha kubadilishia nguo: Minala akiwa na wachezaji wenake wa timu ya vijana ya Lazio
Minala akiwa na mshambuliaji wa Udinese, Antonio Di Natale
Minala akiwa chumbani kwao
Minala alichezea Napoli na Inter kabla ya kujiunga na The Romans

Utetezi: Wakala wa Minala amesema mchezaji huyo anaonekana mzee kwa sababu ya tabu za maisha alizopitia utotoni
Kwanja: Amelazimika kufuta akaunti zake za Instagram na Facebook, lakini amebaki kwenye Twitter tu
Wakala wake, Diego Tavano, ameliambia gazeti la michezo, La Gazzetta kwamba; "Alikuwa na wakati mgumu katika makuzi yake. Ikiwa utazungumza naye,utakubali kwamba ana umri wa miaka 17 kweli,".
Minala bado ana akaunti ya Twitter na baada ya sakata la umri wake,akaandika ujumbe usemao: "Roho mbaya ni udhaifu wa mtu, nao hao wenye roho mbaya inawaumawakikukuona upo Serie A. Nakupenda! Forza Lazio,".



.png)
0 comments:
Post a Comment